Tuesday, 24 March 2015

LOWASSA,MAKAMBA ELEWENI HAYA........

Wagombea uraisi kujibizana kwa kukosana harakati wanazozifanya ili kufikia malengo yao ya kushika nafasi ya juu zaidi ya kuongoza nchi hii iliyojaa maziwa na asali ni kujishushia heshima kulingana na nafasi wanayoitaka ni ya heshima na inayoitaji utii na hekima ya hali ya juu. Hivi karibuni watanzania tumeshuhudia wagombea kadhaa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ie mbunge wa Monduli na Aliekuwa waziri mkuu Edward Lowassa na mbunge wa bambuli ambae pia ni Naibu waziri katika sekta fulani hapa nchini inayohusika na masuala ya sayansi na teknolojia wakifanya harakati za wazi kuonyesha uwezo wao. Lowassa amekuwa akipoke makundi mbalimbali anayodai/yanayodaiwa kumuomba achukue fomu ya kugombea nafasi hiyo huku mpinazani wake ndani ya chama chake ndg J Makamba na team(wafuasi) yake ikishutumu kuwa Lowassa anaratibu kwa kuhonga. huku maswali yakibaki kwa wanachama na wananchi je? Lowassa anayo jeuri ya pesa kiasi cha kuhonga mamia ya watu?.... Januar Makamba nae amekuwa akiandika vitabu kufanya vipindi maalumu (#MindSpeak) Ambapo yote yamekuwa yakiweka maswali kwa team nyingine zinazonyemelea nafasi hiyo. Inaonekana Makamba na Lowassa wanatumia upungufu wa mwenzake bila kujua kuwa Watanzania waleo tumebadilika na hatukupi kisa wewe ni kijana au kwa kuwa wewe una jeuri ya pesa. Naweza Kusema harakati mnazoendeleza watanzania wanaziona kama mbio za sakafuni, huku chama pinzani wanachukulia kama vita vya panzi. Kaka Makamba Na Baba Lowassa kuendeleza harakati sio vibaya ila kuponda harakati za mwezio ndio mapungufu yalipo. nawasihi ukiona mapungufu ya mwenzio yatumie kama