Saturday, 29 August 2015

Kikwete asema kaulii zinazotolewa na upizani kuwa na uchochezi


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amesema baadhi ya kauli zinazotolewa na Umoja wa Vyama vya Upinzani (Ukawa), zinaashiria uvunjifu wa amani pindi matokeo ya kura yatakapoanishwa baada ya zoezi la upigaji kura Oktoba 25 mwaka huu.

Rais Kikwete alisema baadhi ya kauli hizo zimekuwa zikionyesha wazi viashiria vya uvunjifu wa amani na upotoshaji kwa kundi kubwa la vijana ambao wanapiga kura kwa mara ya kwanza.

Akizungumza wakati akizindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao jijini Dar es Salaam Rais Kikwete alisema;

“Wamediriki kusema wazi bila kificho kwamba patakuwa hapatoshi, hizi ni kauli zinazoashiria uvunjifu wa amani. Tunachokisema CCM ushindi kwetu ni lazima na tutashinda kwa kishindo na kwenda nginja nginja mpaka Ikulu.”

Kikwete alisema CCM imejipanga kuhakikisha inapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao na kuongeza kuwa ili kufanikisha hilo wamepanga kikosi kazi ambacho kitatembea nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, mtu kwa mtu ikiwa kwa sasa tayari wameshaanza kufanya kampeni zao kupitia mtandao ya simu za mkononi.

Katika hafla hiyo ya kuzindua kampeni hiyo inayoratibiwa na msanii wa filamu na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, Rais  Kikwete aliwataka wanawake kaungalia mazuri yote yaliyofanywa na Serikali ya CCM katika kumuinua mwanamke.

Source:mwananchi

Waandamanaji wananaopinga serikali wakusanyika Malaysia


Maelfu ya waandamaji wanaopinga serikali wamekusanyika katika nji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur wakitaka waziri mkuu Najib Razak ajiuzulu kwa madai ya ufisadi yanayomkabili.

Mkutano huu wa hadhara umekuwa ukiendelea kwa siku mbili sasa hata baada ya polisi kuupiga marufuku.
Waandamanaji hao pia walikiuka amri rasmi ya kutovaa nguo za manjano zinazotumika na kundi ambalo limeandaa maandamano hayo.

maandamano hayo yalianzishwa baada ya zaidi ya dola milioni mia moja kupatikana katika akaunti ya kibinafsi ya waziri mkuu. Amesisitiza kuwa pesa hizo zilikuwa za msaada na akakanusha kufanya kosa lolote.



Source: bbcswahili

Mahakama moja Misri yawahukumu jela waandishi watatu wa aljazera.


Mahakama ya Misri imewahukumu waandishi watatu wa kituo cha runinga cha Al jazeera kwenda jela miaka mitatu.

Hukumu hiyo ilitolewa baada ya waandishi hao Mohamed Fahmy, Peter Greste na Baher Mohamed kupatikana na hatia ya kutangaza habari za uongo na kulisaidia kundi la Muslim Brotherhood ambalo kwa sasa linatambuliwa kama kundi la kigaidi.

Baher Mohamed pia alihukumiwa kifungo kingine cha miezi sita.

Hata hivyo mmoja wa waandishi hao Peter Greste, yuko nje ya nchi hiyo baada ya kutimuliwa kutoka nchini kwake tangu mwezi Ferbruari.


Licha ya Nick Minaj kuponda tuzo za MTV amepewa nafasi hii. endelea……


Siku ya jumapili agust 30 ni kilele cha tuzo za MTV kwa wanamuziki wa Marekani na tayari wasanii watakao panda siku hiyo wameshajulikana.

Pamoja na Nicki Minaji kuponda uteuzi wa wasanii ndani ya tuzo hizo mwaka huu, lakini uongozi wa MTV umempa shavu Niki Monaji na yeye ndiye msanii atakaeanza kufanya show siku hiyo.

Nicki Minaj anaungana na baadhi ya wasanii wenzake waliotajwa kufanya onyesho siku hiyo ambao ni Justin Bieber, Mackelmore, Ryan Lewis, Pharrell Williams, Tori Kelly ,A$AP Rocky, Twenty One Pilots, Demi Lovato naNick Jonas.


Tuesday, 25 August 2015

Tunatishwa kisa tumeama chama. Ni kutoka Kilimanjaro




Baadhi ya waliokuwa viongozi wa chama cha mapinduzi waliohamia chama cha demokrasia na maendeleo Chadema mkoa wa Kilimanjaro wamesema wameanza kupokea vitisho vya kuhatarisha usalama wa maisha yao ikiwemo kutekwa na kuteswa.

Hayo yamebainishwa na aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro Bw.Fredy Mushi na aliyekuwa katibu wa fedha na uchumi CCM mkoa wa Kilimanjaro Bw.Paul Matemu wakati wakikabidhiwa kadi za baraza la vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo katika manispaa ya Moshi.

Wamesema pamoja na vitisho ambavyo wameanza kupokea hawataogopa na kwamba wamejiandaa ipasavyo kufanya kampeni za kistaarabu ili kuhakikisha wanapata viongozi bora wenye sifa na kufikia lengo la kuleta mabadiliko ya kweli kupitia vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi(UKAWA).

Mapema akikabidhi kadi kwa wananchama hao mwenyekiti wa baraza la vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema)katika manispaa ya Moshi Bw.Dominick Tarimo amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuahidi kufanya kampeni za kistarabu bila vurugu ili kuhakikisha uchaguzi ambao unatarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu unamalizika kwa amani na utulivu.

Naye katibu wa baraza la vijana Chadema Bw.Deogratius Kiwelu amewataka viongozi wanaotoka chama cha mapinduzi na kujiunga  na chama hicho kufuata sheria na kanuni za chama hicho ili kupata ushindi wa kishindo kuanzia ngazi ya uraisi, wabunge na madiwani.

Anguko la soko la hisa bara asia.


Dunia inamkia siku nyingine ya anguko la soko la hisa huko bara la Asia ambapo Japan katika soko kubwa kabisa duniani la hisa limeanguka leo hii huku kukiwa na hofu ya kuporomoka kwa uchumi nchini China.


Soko la hisa la Japan limeanguka kwa asilimia tatu leo jumanne, huko nako nchini Australia soko la hisa likianguka.

Wawekezaji wamekuwa na wasi wasi kutokana na kuanguka kwa soko la hisa huko china ambalo limeanguka kwa asilimia nane nukta tano anguko ambalo ni kubwa kutokea tangu mwaka 2007.




Chanzo:bbcswahili