Friday, 17 July 2015

#Kilimanjaro: Full ripoti ya ajali iliyosababisha vifo vya watu wanne.

 Fuso na baadhi ya mashuhuda waliokuwa katika eneo la tukio


Mwonekano waHaice iliyokuwa na abiria, mara baada ya tukio

Watu wanne wamefariki dunia na wengine kumi na moja kujeruhiwa vibaya baada ya gari aina ya fuso iliyokuwa imebeba mchele kugonga Haice iliyokuwa imebeba abiria kwa nyuma katika eneo la daraja la mto Kikavu wilayani hai mkoani Kilimanjaro.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro SACP Fulgence Ngonyani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imehusisha gari aina ya Haice iliyokuwa imebeba abiria ikitokea Sanya Juu kuelekea mjini Moshi na fuso hiyo iliyokuwa imebeba mchele ikitokea mkoani Shinyanga kuelekea mjini Moshi.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kwamba dereva wa fuso ambaye hajafahamika jina lake ametoroka baada ya kutokea kwa ajali hiyo na kwamba eneo hilo ambalo ajali hiyo imetokea kuna mteremko mkali.

Baadhi ya majeruhi waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC kwa matibabu na baadhi ya mashuhuda wameelezea chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa dereva wa gari aina ya fuso kuendesha gari kwa mwendo kasi katika eneo hilo ambalo lina vielelezo vinavyo onesha eneo hilo ni hatari.

Kwa upande wake mganga mkuu idara ya mapokezi katika hospitali ya rufaa ya KCMC Dkt Noel Makundi amesema jumla ya majeruhi saba waliofikishwa katika hospitali hiyo majeruhi wanne hali zao ni mbaya zaidi.



Pata update zote ungana nami instagram,facebook na twitter @ShadrackMafie

#Arusha: Mradi wa ujenzi wa kituo cha kupima hali ya hewa umeaza kutekelezwa katika wilaya ya Meru.

Bodi ya maji ya bonde la mto pangani yenye ofisi zake wilayani Moshi,Imeanza kutekeleza  mradi wa ujenzi wa  kituo cha hali ya hewa katika wilaya ya Meru

Akizungumza na  Shadrack Mafie mhaidrolojia wa bodi hiyo ndg. Bakari Mohamed Bamba amesema kulingana na jeografia wamelazimika kujenga kituo hicho katika kijiji cha Mareu,kata ya King'ori wilayani humo.kadhalika alisema kituo hicho kitatumika kupima kuongezeka na kupungua kwa maji katika Mito.

Pia ndg Bakari aliongeza kwa kuainisha lengo la mradi kuwa ni kuwasaidia wananchi na wakaazi waishio mabondeni kwa kuwa historia inaonyesha mvua nyingi zinazonyesha katika maeneo ya ukanda wa juu ndizo zinazosababisha madhara katika maeneo ya  Makiba,Malula na maeneo mengine ya ukanda wa chini.

Bwana Bakari pia alimaliza kwa kuwasihi wote watakaonufaika na mradi watumie vyema taarifa zitakazotolewa na kituo


Ungana nami√√√√



Liverpool yatenga pauni milioni 32.5 kwa Aston villa

Baada ya Klabu ya Liverpool nchini Uingereza kupokea kitita cha pauni milioni 49 kutoka kwa klabu ya Manchester United kutokana na mauzo ya mchezaji Raheem Starling,imetoa kitita cha pauni milioni 32.5 kwa Aston Villa kwa lengo la kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alifunga mabao 12 katika mechi 12 katika msimu wa mwaka 2014-2015 na kuisadia Villa kusalia katika ligi kuu ya Uingereza.

Ikumbukwe Benteke bado amesalia na kandarasi ya miaka 2 katika klabu ya Villa.



#ShadyComTz