Tuesday, 31 March 2015

KUELEKEA KURA YA MAONI YA KATIBA PENDEKEZWA.....TUCHAMBUE PAMOJA

Kufuatia kura ya maoni ya katiba pendekezwa. Kwa mujibu wa ratiba za serikali na taarifa tulizonazo wananchi wa tanzania wenye umri uliothibika kuwa na uwezo wa kupiga kura yaani umri wa miaka 18 na kuendelea tarehe 31th April Mwaka huu tutaenda kwenye hatua ya kuipigia katiba pendekezwa kura ya kuikubali au kuikataa licha ya changamoto zilizopo, ambazo ni mkanganyiko wa hatma ya kujiandikisha kwa wenye sifa kwa muda uliobaki wa siku chache zijazo,Pili asilimia nyingi au wastani waoenda kupiga kura kutokupata nakala za rasimu pendekezwa, Tatu kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba kungepaswa hadi leo ziwepo team mbili zitakazo ratibu kampeni ya wanayokubali na ya wanaokataa.. Tukiachana na hayo tupate kutazame katiba pendekezwa kidogo. kiukweli katiba pendekezwa imetazama vya kutosha umuhimu wa haki za binadamu katika ibara 36 Hadi Ibara Ya 59. imeainisha vyema haki za binadamu na kuzitafsiri vema.. Katika mapungufu ya katiba hii pendekezwa ambayo inasubiri hatua ya reforendum. Moja: Tutazame ibara ya 124 kuhusu serikali za mitaa. katika ibara hii kiukweli nilitegemea ingetaja sifa za watendaji katika kila ngazi.ila katiba pendekezwa haina sifa hizi. Pili: Tutazame ibara ya 121 kuhusu katibu mkuu kiongozi. Ibara hii imeainisha mamlaka ya katibu mkuu kiongozi kuwa ni 1. Katibu wa baraza la mawaziri. 2. katibu wa usalama wa taifa. 3. mwenyekiti wa kamati maalumu ya makatibu 4. mkuu wa utumishi wa umma. Ukitazama upatikanaji wa katibu mkuu huyu unaleta mashaka sana kwa kuwa atatokana na makatibu wengine ambapo ni jambo la kustajabisha kuwa mtu huyu atawezaje kumudu kazi zote zaidi ya makatibu wenzake?. Nne: sifa za mbunge. rasimu ya Tume iliona umuhimu wa wabunge wa kutunga sheria, kuishauri na kusimamia serikali, Ikaweka kigezo cha elimu. ila katiba pendekezwa imeweka kigezo cha kujua kusoma na kuandika pekee huku ikisema mawaziri watatokana na wabunge. hapa napata maswali mengi sana. baadhi ni:- 1. endapo asilimia kubwa ya wabunge watakaochaguliwa watakuwa wanajua kusoma na kuandika pekee tutakuwa na mawaziri wa dizaini hiyo hiyo?. jibu ni ndio. 2. endapo tutatungiwa sheria na watu wanaojua kusoma na kuandika pekee nani ataiingiza katika mfumo wa lugha ya kizungu?. sina jibu hapa. 3. endapo itakuwa ni kujua kusoma na kuandika pekee je bajeti nani atatusaidia kupanga? hili linakuja baada ya kupata uongozi wa serikali (mawaziri) anaejua kusoma na kuandika pekee.. Wengi Tumezoea Kuongelea Muundo Wa Muungano Pekee. Ila Katiba Pendekezwa Ina Madhaifu Mengi... Haya Ni mawazo yangu kwa katiba pendekezwa na nimepost leo kwa sheria inaniruhusu na kukuruhusu kujadili katiba pendekezwa pia zimebaki siku zinazotakikana kwa sheria ya mabadiliko ya sheria... Tuendelee Kuichambua Katiba Pendekezwa Tuchekiane Kwenye Twitter @shadrackmafie.