Friday, 6 February 2015

INATIA HASIRA UKIYAFIKIRI NA KUYATAFAKARI LAZIMA UFANYE MABADILIKO

Tanzania Ni Jina La Nchi Lililoundwa Baada Ya Nchi Mbili Kuungana, Nchi Hizi Mbili Ni Tanganyika Na Visiwa Vya Zanzibar. Tanzania Inasifika Kwa Amani Iliyotukuka Inayoenziwa Kila Siku Tangu Mwanzo Wa Tanzania. HASIRA YA MTANZANIA Ukitazama Historia Ya Kiuongozi Na Utekelezaji Wa Katika Miaka Yote Tangu Kuzaliwa Kwa Tanzania Utagundua Yafuatayo. Ongezeko La Vitendo Vya Ukwapuaji Wa Fedha Za Umma. Ambao Ukwapuaji Huu Unahusisha Watu Wanaoaminika Na Kupewa Nafasi Za Kiutawala. Hali Iliyofanya Wananchi Kuwachukia Viongozi Wao Na Kupoteza Imani Na Yeyote Atakaetaka Fursa Ya Kuongoza. Wananchi Wamejenga Nia Ya Kutafuta Mfumo Madhubuti Utakaonusuru Taifa Kwa Kuwa Inafikirika, Kusemwa Na Kuhisiwa Chama Kilichopewa Dhamana Ya Kuunda Serikali Kimeshindwa Kwa Kuwa Chama Hicho Kimeunda Serikali Inayoshindwa Kusimamia UCHUMI (deni La Taifa Na thamani Ya Sarafu Yetu), RASILIMALI ( Madini, Misitu, Bahari, Watu, Arthi Nk) SIASA SAFI Nk. Pia Kitendo Kingine Kilicho hatari Sana Ni Kitendo Cha Urafiki Baina Ya Raia Na Polisi Na Urafiki Baina Ya Raia Na Viongozi Kumejengwa Daraja Kubwa Ambalo Linafanya Watanzania Kushindwa Kuwaeleza Na Kuwafikishia Ujumbe Unaowapasa Mf> Mh Mbowe Amekuwa Akisema Mara Kadhaa Kuwa "ninao Ushaidi Wa Alietega Au Kurusha Bomu Katika Mkutano Wa Chadema Arusha Na Satotoa Ushirikiano Kwa Polisi Kwa Kuwa Wanahusika Kwa Upande Fulani". Hii Ni Hatua Mbaya. Kingine Kikubwa Zaidi Ni Jeshi La Polisi Kutumia Nguvu Kubwa Zaidi Inasababisha Nchi Kuwa Na OmbaOmba (dependent Person) Wengi Kutokana Na Kufanywa Walemavu Na Wengine Kufa. Ni Baadhi Hoja Za Watanzania Kukata Tamaa Na Mfumo (System) Wa Serikali Yetu Sikivu Au Isiyo Sikivu..

STORI MBILI GUMZO ZILIZOTOKEA JANA

Jana Tarehe 5/2/2015 Kulikuwa Na Kauli Mbalimbali Zilizosababisha Watu Kuzua Majadiliano Makubwa Kwenye Mitandao Ya Kijamii Na Nje. Kauli Hizo Ni Kama Ifuatavyo. 1.Jana Katika Kipindi Cha Maswali Na Majibu Bungeni Mh Suzan Lyimo Aliuliza Swali Kuhusu Suala La Almashauri Ya Ruvuma Kuandika Barua Kwa Shule Zilizopo Katika Almashauri Kushurutisha Mwalimu Na Wanafunzi Kuudhuria Maadhimisho Ya Miaka 38 Ya CCM. Swali Ambalo Waziri Mkuu Alisema Kuwa Wale Ni Watoto Wa WanaCCM Hivyo Hakuna Makosa.(Mtoto Wa Nyoka Ni Nyoka).Majibu Haya Hayakuridhisha Kitendo Kilichozaa Majadiliano Makubwa Hasa Katika Blogs Na Twitter. 2. Bungeni Mh Eliatonga Mrema Mbunge Wa Jimbo La Vunjo Alitoa Taarifa Binafsi Ambayo Ilionekana Kumshtumu Mh Mbatia Mbunge Wa Kuteuliwa, Kwa Kusema "Nilipokuwa Natibiwa India Mh Mbatia Alinukuliwa Na Gazeti La Mwananchi Akiwaambia Wananchi Wa Jimbo Langu Kuwa Wasinichague Kwa Kuwa Mimi Naumwa Ukimwi Na Nitakufa Nasema Hafi Mtu Hapa." Pia Ripoti Hii Ya Afya Ya Ilizua Gumzo. Ni Wakati Wa Wahusika Haswa Hawa Viongozi Kupima Maneno/Majibu Wayatoayo Katika Mazungumzo.

Wednesday, 4 February 2015

MASAHA KABLA YA UCHAGUZI MKUU 2015

Ni Mwiaka 53 Tukiwa Tunaongozwa Na Serikali Inayoundwa Na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Katika Awamu Nne, Awamu Ya Kwanza Tuliongozwa Na Hayati Mwl Julias Kambarage Nyerere Awamu Hii Ya Kwanza Ilikuwa Ya Kusifika. Awamu Ya Pili Tukawa Na Mh Mwinyi Mzee Wa Ruksa. Awamu Ya Tatu Mh Benjamin Mkapa Ambae Alisifika Kwa Kuimarisha Uchumi, Japo Wananchi Walianza Kupoteza Imani Na Chama. Na Katika Awamu Hii Tuliyonayo Tupo Na Mh Jakaya Kikwete Ambae Amepata Changamoto Nyingi Zilizowafanya Wengi Kukata Tamaa Na Chama Hiki Kilichoridhi Damu Ya TANU Iliyotutafutia Uhuru Kutoka Kwa jkkWakoloni. Ni Nafasi Yetu Kutafakari Ni Uongozi Upi Unatufaa. ANGALIZO KWA VYAMA. 1.Kutokana Na Wananchi Wa Tanzania Kuelimika Na Kuwa Wachunguzi Wa Hali Ya Juu Yapasa Chama Kijipange Kwa Sera Zinazotekelezeka. 2. Chama Chochote Cha Siasa Kumwandaa Mgombea Anaetarajiwa Na Wengi Na Kuungwa Mkono Ili Kuweza Kupata Ushindi Usio Na Doa. 3. Chama Chochote Kiandae Na Kufanya Kampeni Zake Kistaharabu Pasipo Kuingiliana Kwa Namna Yoyote Ile Itakayosababisha Uvunjifu Wa Amani. 4. Chama Chochote Kihakikishe Wapiga Kura Wanapata Haki Ya Msingi Ya Kujiandikisha Kwa Kutoa Elimu Zaidi.( Kwa Kuzingatia Tutakuwa Na Mfumo Mpya Wa BVR). 5. Chama Chochote Kielewe Kinaongea Na Watanzania Wasomi Ambao Wanahoji Kila Herufi Itokayo Mdomoni Kwa Mgombea Au Kiongozi. Hapa Namaanisha Kuongea Pasipo Kuropoka. 6. Chama Chochote Kiwe Tayari Kujibu Maswali Magumu Yatakayojitokeza Popote Kukiusu,Ikiwemo Kwenye Mitandao Ya Kijamii. Hii Itakisaidia Kuaminiwa. 7. Chama Chochote Kiwe Na Utoaji Wa Elimu Maalumu Ya Kuheshimu Na Kutii Sheria.Pia Walitake Jeshi la Polisi Kufanya Kazi Katika Taratibu Na Sheria. 8. Chama Chochote Kikiona Makosa Popote Kitoe Msahada Ili Kuweza Kupatia Ufumbuzi Ambao Utafanya Kila Kitu Kiwe Sawa Kama Kilivopangwa. 9. Chama Chochote Kijitaidi Kutumia Lugha Inayoeleweka Katika Utoaji Wa Sera Ili Kundi Kubwa Liweze Kuelewa Na Kuzichambua. Kitendo Hiki Kitafanya Kila Mtu Ajue Anapigia Nini Au Nani Na Kwa Sababu Gani. 10. Ni Vema Na Sisi Raia Tukawa Watulivu Katika Kuitafuta Tanzania Iliyo Bora Itakayokua Mfano Wa Kuigwa Katika Nyanja Zote. Uchumi Imara, Siasa Bora, Ulinzi Na Usalama Ulioimarika NK