Saturday, 20 February 2016

Kwa wale ambao bado hawajapata kutazama matokeo kidato cha nne 2015 haya hapa.

Ni mara kadhaa nimekuwa nikiulizwa link ya kupata matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa Tar 18 Feb 2016. Sasa basi Mabibi na mabwana unaweza kuyapata kwa BOFYA HAPA

Vijana wa skauti watupiwa macho na Mh. Magufuli.



Serikali inaangalia uwezekano wa kuanza kuwatumia vijana wa skauti katika vyombo vya ulinzi na usalama huku ikiwaagiza wakurugenzi wa halmashauri kuwaruhusu walimu kushiriki katika shughuli za skauti.

Hayo yameelezwa na Rais DR. JOHN POMBE MAGUFULI katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa DKT HUSEIN MWINYI na pia kuagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinavilinda kikamilifu vyama vya skauti ili visife bila sababu za msingi.


Rais wa Skauti Tanzania Profesa JOYCE NDALICHAKO ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi licha ya kupongeza juhudi kubwa zinazofanywa na uongozi mpya wa skauti kukiimarisha chama hicho, amesema ni vema chama kikaangalia uwezekano wa kuongeza wigo wa kuwapata vijana wengi zaidi.


Akitoa maelezo ya utendaji kazi wa chama hicho tangu uanze uongozi mpya mwaka 2013, Kamishina Mkuu wa Skauti Tanzania ABDULKARIM SHAH amesema kazi kubwa wanayoifanya  kwa sasa ni kuhakikisha wanarejesha heshima ya chama hicho iliyokuwa imepotea kwa miaka kadhaa.


Chanzo: ITV Tanzania

Fursa: Johari anatafuta kijana wa kiume (Mchumba) wa kuwa nae maishani.




Mwigizaji mkongwe wa Bongo movie Blandina Chagula 'Johari' amesema kwa sasa anatafuta kijana wa kuwa naye katika maisha.


 "Mimi kwa sasa nipo mwenyewe (Single) akitokea kijana mwenye malengo na mwenye dhamira ya kweli nipo tayari kuwa naye"  amesema Johari

Majungu yanaturudisha nyuma wasanii wa kike- Lina.


Mwanadada kunako muziki wa Bongo fleva, Linah Sanga, ametoa yaliyo moyoni kwa kuweka wazi kuwa wasanii wengi wa kike hapa Bongo wameshindwa kufanikiwa kwenye muziki kutokana na kuendekeza majungu badala ya kufanya kazi.
Linah amesema kitendo hicho kimekuwa kikiwarudusha nyuma na kusema ni wakati sasa kwa wasanii wa kike kujitafakari na kufanya kazi kwa ushirikiano.
Mwanadada kunako muziki wa Bongo fleva, Linah Sanga, ametoa yaliyo moyoni kwa kuweka wazi kuwa wasanii wengi wa kike hapa Bongo wameshindwa kufanikiwa kwenye muziki kutokana na kuendekeza majungu badala ya kufanya kazi.
Linah amesema kitendo hicho kimekuwa kikiwarudusha nyuma na kusema ni wakati sasa kwa wasanii wa kike kujitafakari na kufanya kazi kwa ushirikiano.

Msanii Juma Nature amefunguka umuhimu wa mashabiki wake. Soma zaidi

Juma Nature

Msanii mkongwe katika gemu ya muziki hapa nchini msanii Juma Nature akizungumza na Times FM ameweka bayana kuwa mashabiki wake ndio wanamfanya aonekane bado yupo juu.

"Mashabiki ndio wananifanya nisishuke kimuziki inawa wapo baadhi ya watu wanasema nimeshuka haa kufkia hatua ya kutokutaka kufanya kazi na mimi , lakini ukweli ni kwamba bado ipo fiti" ameweka bayana Juma Nature

Aliongeza kuwa kujiamini na kuwa na nidhamu ya kikazi ndio inawafanya mashabiki wake kmpenda na kukumbushia kuwa uwezo wake wa kkazi ndio uliomfamya aweze kufaikisha tamasha alilowahi kufanya la ktimiza miaka 16 kwenye fani"

Ikumbukwe msanii Juma Naturealitoa nyimbo yake wiki moja iliyopita unaoenda kwa jina la " Kidaluso" pia vymbo kadhaa vya habari vilimnuuu akisema kuwa anatarajia kufanya kolabo na msanii Yemi Alade kutokea nchini Nigeria.

Hii ni kauli ya Ali Kiba kuhusu ushindani anaoupata katika sanaa ya bongo fleva


ALIKIBA1
Staa wa bongo fleva Ali Kiba amekiri kuwa ushindani uliopo sasa kwenye muziki wa bongo fleva umemfanya arekebishe vitu kadhaa kwenye muziki wake hii ni pamoja na kufanya video zenye viwango zaidi.
Licha ya kauli yake hiyo Ali Kiba ameweka wazi kuwa ushindani haupo kabisa kwenye akili yake,yaani yeye hashindani na mtu yeyote yule.

Chanzo: Clouds