Msemo mmoja husema "ndege wa rangi moja huruka pamoja" lakini tafsiri ya msemo huo sioni ikitimia ndani ya Ukawa hasa kwa mkoa wa Arusha.
Ni mara nyingi sasa viongozi wa vyama vya upinzani jijini Arusha wamekuwa wakipishana kauli. Tena kwa kutumia vyombo vya habari na kwenye mikusanyiko,wengi wakionyesha nia ya kuhitaji kuziongoza kata mbalimbali mkoani Arusha.
Swali la wengi linaangukia kwa UKAWA kwa ujumla wake.
Tafsiri ya Ukawa ni umoja wa katiba ya wananchi ambayo nayo iliyopendekezwaimezua mipishano ya kauli. Ninalojadili siyo hilo nalenga zaidi mchakato wa kutafuta wagombea wa vyama hivi vilivyoongeza majukumu ya ukawa kutoka kwenye Katiba hadi Kuungana ili kuking'oa chama kilichopo madarakani. Wasiwasi unakuja baada ya maneno mengi yaliyotofautiana kuhusu kugawana kata kwa vyama hivyo vinavyounda Ukawa. Bado ni usiku ila majogoo yameshaanza kuwika, sijui ikifika asubuhi jogoo watafanya nini. Ni swali ambalo majibu yake yataonekana pakikucha.
Ni wazi kuwa majimbo kadhaa Arusha tayari yanaongozwa na upinzani. Je inawezekana kwa mti usio na mzizi kuwa na matawi? Hilo ni la kujiuliza kwa vyama vingine ndani ya UKAWA Arusha. Yaliyosikika yanashangaza na yanashindwa kufafanua nafasi ya Ukawa kwenye uchaguzi mkuu ndani ya Arusha. Wapo wanaodai kuwa ukawa arusha ulikosekana toka uchaguzi wa serikali za mitaa huku viongozi wengine wakisema mchakato wa ukawa kufanya mchujo wa kupata wagombea atakayesimama kama UKAWA upo. ni kauli zenye utata na swali langu ni je kwa hali hiyo malengo ya Ukawa yatatimia ndani ya Arusha? Majibu yatapatikana muda unavyozid kwenda.
Siasa za Tanzania ni kweli kuwa zinakua lakini tafsiri yake haieleweki kwa wote. Mara leo fulani katimuliwa ndani ya Chama, mara chama kipya chaanzishwa, mara huyu kaombwa agombee yote ni sawa ndani ya siasa kwa kuwa vipo ndani ya mujibu wa Sheria. Ila kubwa unahitajika umakini mkubwa wa kutafsiri yale yote yanayoendelea, hatujui kama malengo ya vile tunavyoviona ni kuikomboa Tanzania kwenye nyanja mbalimbali za kimaisha.Busara pia zinahitajika kwani hata makundi ya dini nayo yameonyesha kujihusisha moja kwa moja kisiasa bila kujali athari zinazoweza kujitokeza, Cha msingi Watanzania tumuombe Mungu afanikishe yote yaliyo mbele yetu na kwa juhudi zetu wenyewe tudumishe amani upendo na mshikamano.
Mungu ibariki Tanzania