MICHEZO NA BURUDANI

Hii ndiyo kauli ya Rapper Ney Wamitego kuhusu kufanya filamu na msanii Diamond




Rapper huyo ameuambia mtandao mkubwa hapa nchini ujulikanao kama Bongo 5 kuwa baada ya kuharibika kwa mipango ya filamu ya Salam Zao, alipanga kufanya kitu kikubwa akiwa na Diamond.

“Nilikuwa na idea ya kufanya movie kubwa na tuliwahi kukaa team yangu pia nakumbuka tulishawahi kukaa na Diamond, tukasema tukija kufanya movie tunaweza tukaja kuuza sana. Sasa tatizo ni timing na mtu ambaye mimi nilikuwa namtegemea.”

“Ni mtu kutoka nje ili iwe ni movie kubwa kuliko movie yoyote ile. Yeye alikuwa ni Mjerumani na kwa kipindi hicho nilikuwa na mahusiano naye ila alivyorudi kwao hakurudi tena. Lakini tulikuwa tuna kitu kizuri zaidi, hatukutaka kufanya movie ya ilimradi movie, so time ikifika tukiwa tupo free tutakifanya tulichokipanga,” alisema Nay.

No comments:

Post a Comment