Friday, 4 September 2015

Mbaroni kwa kuzidisha dakika 6 katika muda kufanya kampeni.




MGOMBEA ubunge wa Chadema, Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, jana amekamatwa na polisi akidaiwa kuzidisha muda katika mkutano wake wa kampeni na kufanya maandamano bila kibali.

Tukio hilo lilitokea baada ya mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro ambapo Lema alihutubia hadi saa 12:06 badala ya saa 12:00, na aliposhuka jukwaani na kuanza kuondoka, wafuasi wake walianza kumfuata na kusukuma gari lake.

Baada ya hatua chache kutoka uwanjani hapo, polisi walianza kuwatawanya wafuasi hao na baadaye kumkamata Lema na kwenda naye Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Arusha.

Awali katika hotuba yake, Lema alimshukia mpinzani wake, Philemon Mollel wa CCM, kwamba anafanya kampeni zake kwa kutumia mbinu chafu za ukabila na udini.

Katika uzinduzi wake wa kampeni Agosti 23, mwaka huu, mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, alizidisha dakika 36, lakini hakuna hatua yoyote aliyochukuliwa.

SOURCE; MTANZANIA

Wednesday, 2 September 2015

Ijue Zanzibar na vivutio vyake




Na, Baraka Ngofira


Mji mkongwe wa Zanzibar ni mji wenye historia kubwa na jina kubwa sana hasa kwa kusifika katika biashara ya utumwa ambapo kulikuwa na soko kuu la Afrika Mashariki la kuuzia watumwa kutoka katika nchi zinazozunguka Afrika ya mashariki.


 Historia haiishii kutaja tu kama mji huu ni maarufu katika uuzaji na usafirishaji wa watumwa bali pia mji huu unasifika kwa kuwa na watu wengi maarufu ambao kusahaulika katika historia ya dunia ni vigumu kama vile sultan Seyyid Said, Tippu Tip, Siti binti Said ambaye alivuma kwa uimbaji wa taarabu za Kiswahili, pia wapo Shekh Abdallah saleh Farsy ambaye ni mwandishi wa vitabu maarufu na mtafsiri wa Quran katika lugha ya Kiswahili.
Mji huu mkongwe wa Zanzibar sio tu unasifika kwa historia ndefu bali pia ni mji ambao umeingizwa kwenye urithi wa dunia ukiwa na fukwe nzuri za kuvutia, maboma ya kuvutia na yaliyojaa maajabu ikiwemo jumba linalofahamika kama Beit-al-ajaib katika lugha ya kiarabu umaajabu wa jumba ili ni kuwa na nguzo 44 zilizojengwa  kwa umahiri na umaridadi na uimara wa hali ya juu.


Jambo la kufurahisha na kuvutia katika jingo hili ndilo jengo la kwanza Afrika Mashariki na kusini mwa jangwa la sahara kuwa na umeme na lifti, na hivyo kulifanya kuwa jumba la kitalii linalovutia watalii na watu wengine wafikao Zanzibar kwenda kutalii na kutazama jengo hili.
Pia limekuwa kivutio kikubwa kwa watalii kuja kujifunza tamaduni na mambo ya kale na hatua mbalimbali za kimaendeleo zilizo kuwa zikifanyika Zanzibar kwa kale na zinazo endelea mpaka sasa, kwa kweli ufikapo Zanzibar usisite kutembelea kwenye jengo hili la kimaajabu.


Kivutio kingine kinachovutia watu kwenda kutalii Zanzibar ni mji mkongwe wa Zanzibar mji wenye historia kubwa na jina kubwa duniani , mji uliokaliwa na watu wengi, mji wenye majumba mengi ya kitalii , makanisa na misikiti ya kihistiroria yote yanapatikana kwenye mji mkongwe wa Zanzibar.
Nyangumi nao wamekuwa kivutio kikubwa hasa kwa watalii watokao bara na nchi nyingine kuja kupiga picha nyangumi wanaoruka na kuonekana kwa uzuri wakitokea majini na kisha kutumbukia majini. Nyangumi hawa wamewavutia maelfu ya watalii kutembelea Zanzibar na kujionea kwa macho yao na wwengine kubaki midomo wazi wakiwashaa nyangumi hawa jinsi warukavyo na kutumbukia majini, kwa kweli Mungu aliumba ndiyo maneno ambayo uwatoka mara nyingi watu hawa.


Ukiachilia mbali nyangumi uwepo wa fukwe nzuri za kuogelea na kupumuzikia za Kendwa,Mungwi,na kiwengwa ni fukwe nzuri za kuvutia zinazokusanya watu wengi hususani nyakati za jioni na nyakati za sikukuu kama vile za Maulid na zile za Xmass na mwaka mpya . sio tu ni fukwe nzuri pia zina upepo mwanana unaowavutia watu wapate fursa hii hadhimu ya kukaa na wale wawapendao na muda mwingi kubadilisha mawazo.
Pia magofu ya kihistoria , chochoro nazo ni vivutio vikubwa hasa kwa wilaya ya mjini Magharibi ambapo watarii hutumia fursa hii adhimu kutembelea na kushuhudia majengo haya na magofu yaliyojengwa kwa umahili na umaridada na mpaka leo yanahifadhiwa vizuri ili kuendelea kuwavutia watu wote wanaotembelea Zanzibar.


Pia uwepo wa Kima wekundu wanaopatikana kwenye misitu ya Jozani na Ngenzi nao wamekuwa kivutio kikubwa sana hasa kwa watalii wanaofika kutembelea katika misitu hii ya ajabu kujionea wanyama hawa ambao ni adhimu kupatikana bara na katika misitu mingine iliyopo bara na katika nchi nyingine duniani. Kweli maajabu ya kima hawa na rangi zao zimekuwa kivutio kikubwa sana. Uwaangaliapo na hata kupiga picha za kwenda kuonesha watu ambao hawajawahi kuwaaona kima hawa na maajabu yao.

Tuesday, 1 September 2015

Uamisho wa De Gea kwenda Real Madrid wakwama dakika za majeruhi



UHAMISHO wa Pauni Milioni 29 wa Kipa David De Gea kutoka Manchester United kwenda Real Madrid umekwama Dakika za mwisho baada ya Mikataba yake kutokamilika kwa wakati.

Tatizo kubwa ni kuwa Dirisha la Uhamisho huko Spain lilifungwa Jana Saa 7 za Usiku kwa Saa za Tanzania wakati lile la Uingereza Leo ndio mwisho wake, hapo Saa 2 Usiku kwa Saa zetu.

Uhamisho huu wa De Gea ulihusu Kipa huyo kwenda Real na Klabu hiyo ya Spain kuilipa Man United Pauni Milioni 29 pamoja na kumtoa Kipa wao kutoka Costa Rica, Keylor Navas, kwa Man United.

Hivi sasa kila Klabu imebaki kimya lakini ripoti kutoka huko Spain zinadai kuwa Man United ndio waliochelewesha kukamilisha Uhamisho huo kwa kutuma Mkataba uliosainiwa Dakika 1 baada ya Dirisha la Uhamisho kufungwa hapo Saa 7 na Dakika 1 Usiku.

Hata hivyo, habari toka ndani ya Man United zinadai kuwa wanayo Risiti inayoonyesha kuwa Makabrasha yote yalitumwa kwa wakati.

Ikiwa ukweli ni kuchelewa kwa Makabrasha kufika huko Spain kwa wakati basi kilichobaki ni Real kukata Rufaa kwa FIFA ambao ndio wanahusika kwa Uhamisho wa Kimataifa.

Bila hivyo David De Gea atabakia Man United kwa Msimu zaidi hadi Mkataba wake umalizike mwishoni mwa Msimu huu wa 2015/16.

Monday, 31 August 2015

Baada ya Nick Minaj kukutana na Miley Cyrus si akamchimba mkwara. soma zaidi

Nick Minaj (Msanii wa hip hop alichukua tuzo ya video bora ya hip hop -Anaconda)


Miley Cyrus (aliyekuwa MC katika tuzo za MTV)


Moja kati ya vitu vilivyoleta mjadala wakati wa ugawajwi wa Tuzo za MTV kwa upande wa wanamuziki wa Marekani ni pale female rapa Nicki Minaj alipomchana MC wa shguhuli hiyo mwanadada Miley Cyrus.

Miley Cyrus. Na Nicki Minaj walikuwa kwenye ugomvi wa maneno kwa muda mrefu hatimaye wawili hao wakakutana ndani ya tuzo hizo na Miley Cyrus ndiye alikuwa MC usiku huo jumapili august 30.

Nicki Minaj alitwa jukwaani kuchukua tuzo yake ya Video bora ya HipHop (Anaconda) na baada ya kuwashukuru wadau wake alimgeukia Miley Cyrus na kumuuliza kwa nini kila siku anamuongelea vibaya?

Miley Cyrus alizuga na kumpngeza Nicki kwa ushndi huo.Haikuweza kujulikana kama hiyo ishu ilipangwa au la pamoja na kuwa uso wa Nicki ulioekana umekasirika.

Nicki alishuka jukwaani na kuelekea sehemu yake ya kukaa huku ukumbi ukifurika kwa kelele za wageni walifika kutokana na maneno ya Nicki kwenda kwa adui wake Miley Cyrus.

Leo tar 31 Agoust nimekuwekea baadhi ya kurasa za juu magazeti. Endelea