Journalist•| Blogger•| Researcher•| Entrepreneur•| Real patriot•| Prospective husband•| Trapper changes
Tuesday, 20 January 2015
Agizo la Serikali ya Tanzania kuhusu utoaji holela wa vyeti vya kuzaliwa
Mamlaka za nchi zatakiwa kuwa
makini katika utoaji wa vibali vya
wageni wanaoishi nchini ili kupunguza
uwezekano wa kutoa vyeti vya
kuzaliwa kwa watu wasio na sifa.
Waziri wa Kazi na Ajira Gaudensia
Kabaka
Sekretarieti ya ajira nchini Tanzania
imezitaka mamlaka nyingine za
serikali kuwa makini zinapotoa vibali
vya hati ya kuishi nchini pamoja na
vyeti vya kuzaliwa ili kuepusha watu
wasio na sifa hususani wageni
kuajiriwa serikalini.
Katibu msaidizi wa sekretarieti ya
ajira nchini Bw Malimi Muya
ameyasema hayo leo jijini Dar es
salaam wakati akiongea na hotmix
ilipotaka kufahamu kuhusu tuhuma za
raia wakigeni kuajiriwa serikalini.
Bwana Muya ameongeza kuwa Ofisi
yake inahimiza vijana walioko vyuoni
na mashuleni kuchukua masomo ya
sayansi na Technolojia kwakua kwa
sasa fani hiyo ndiyo yenye soko kubwa
la ajiri duniani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment