Wednesday, 18 March 2015

NAPE AZICHAPA NA M/KITI...ARUSHA

Nape Nnauye amemfanyia vurugu kubwa Onesmo Nangole Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha kwa sababu ya chuki za kisiasa tu Umri wa Nape na Nangole haulingani lakini jambo la ajabu Nape anampa maelekezo kwa njia ambayo inaonyesha alidhamiria kumdhalilisha kwa kuwa Nangole anahusishwa na kambi ya Lowassa Nape alianza kumtuhumu Nangole kuwa ameandaa mapokezi hafifu kwa ujumbe wa Sekretarieti ya chama taifa na pia kukiuka itifaki muda wote hasa ziara ya Monduli na Karatu kwa sababu ya njaa njaa zake. Jambo hili liliwakera wengi na hasa baadhi ya makada kutoka UVCCM na Umoja wa wanawake huku Nangole akimwambia Nape awe na nidhamu angalao kwa umri wake kwa kuwa chama hicho wamekipigania na hakuna mwenye hatimiliki Mzee Justine Kaaya aliingilia kati na kuwaambia aibu hii inapaswa kumalizwa kwa kuwa eneo hilo watu walikua wakipita na kumtaka Nape kuomba radhi kitendo kilichomkasirisha na kujibu kuwa hawezi kuwaomba radhi vibaraka wa watu bali anasimamia heshima ya chama na sio kutishwa na mafisadi na vibaraka wao Ndipo Mwenyekiti wa Mkoa Nangole alipomjibu akajifunze siasa kwanza maana hajawahi kushinda uchaguzi wowote zaidi ya kubebwa na pia ni msaliti mkubwa mwanzilishi wa chama na kubeba mikoba ya akiba Renatus Kyabo Ghafla Nape akamrushia ngumi Nangole na kusababisha vurugu kubwa na kumvunjia Miwani Mama Martina Gurtu aliyejaribu kuingilia ugomvi huo huku Nangole akichaniwa Shati Lake Vijana waliokua pale Naura Spring waliingilia kati na kuwatenganisha. Kikao cha ndani ndio kinafanyika jioni hii kikiongozwa na Kinana ili kumaliza swala hili. Chanzo: JamiiForums

No comments:

Post a Comment