Friday, 6 February 2015

INATIA HASIRA UKIYAFIKIRI NA KUYATAFAKARI LAZIMA UFANYE MABADILIKO

Tanzania Ni Jina La Nchi Lililoundwa Baada Ya Nchi Mbili Kuungana, Nchi Hizi Mbili Ni Tanganyika Na Visiwa Vya Zanzibar. Tanzania Inasifika Kwa Amani Iliyotukuka Inayoenziwa Kila Siku Tangu Mwanzo Wa Tanzania. HASIRA YA MTANZANIA Ukitazama Historia Ya Kiuongozi Na Utekelezaji Wa Katika Miaka Yote Tangu Kuzaliwa Kwa Tanzania Utagundua Yafuatayo. Ongezeko La Vitendo Vya Ukwapuaji Wa Fedha Za Umma. Ambao Ukwapuaji Huu Unahusisha Watu Wanaoaminika Na Kupewa Nafasi Za Kiutawala. Hali Iliyofanya Wananchi Kuwachukia Viongozi Wao Na Kupoteza Imani Na Yeyote Atakaetaka Fursa Ya Kuongoza. Wananchi Wamejenga Nia Ya Kutafuta Mfumo Madhubuti Utakaonusuru Taifa Kwa Kuwa Inafikirika, Kusemwa Na Kuhisiwa Chama Kilichopewa Dhamana Ya Kuunda Serikali Kimeshindwa Kwa Kuwa Chama Hicho Kimeunda Serikali Inayoshindwa Kusimamia UCHUMI (deni La Taifa Na thamani Ya Sarafu Yetu), RASILIMALI ( Madini, Misitu, Bahari, Watu, Arthi Nk) SIASA SAFI Nk. Pia Kitendo Kingine Kilicho hatari Sana Ni Kitendo Cha Urafiki Baina Ya Raia Na Polisi Na Urafiki Baina Ya Raia Na Viongozi Kumejengwa Daraja Kubwa Ambalo Linafanya Watanzania Kushindwa Kuwaeleza Na Kuwafikishia Ujumbe Unaowapasa Mf> Mh Mbowe Amekuwa Akisema Mara Kadhaa Kuwa "ninao Ushaidi Wa Alietega Au Kurusha Bomu Katika Mkutano Wa Chadema Arusha Na Satotoa Ushirikiano Kwa Polisi Kwa Kuwa Wanahusika Kwa Upande Fulani". Hii Ni Hatua Mbaya. Kingine Kikubwa Zaidi Ni Jeshi La Polisi Kutumia Nguvu Kubwa Zaidi Inasababisha Nchi Kuwa Na OmbaOmba (dependent Person) Wengi Kutokana Na Kufanywa Walemavu Na Wengine Kufa. Ni Baadhi Hoja Za Watanzania Kukata Tamaa Na Mfumo (System) Wa Serikali Yetu Sikivu Au Isiyo Sikivu..

No comments:

Post a Comment