
Akizungumza na Shadrack Mafie mhaidrolojia wa bodi hiyo ndg. Bakari Mohamed Bamba amesema kulingana na jeografia wamelazimika kujenga kituo hicho katika kijiji cha Mareu,kata ya King'ori wilayani humo.kadhalika alisema kituo hicho kitatumika kupima kuongezeka na kupungua kwa maji katika Mito.
Pia ndg Bakari aliongeza kwa kuainisha lengo la mradi kuwa ni kuwasaidia wananchi na wakaazi waishio mabondeni kwa kuwa historia inaonyesha mvua nyingi zinazonyesha katika maeneo ya ukanda wa juu ndizo zinazosababisha madhara katika maeneo ya Makiba,Malula na maeneo mengine ya ukanda wa chini.
Bwana Bakari pia alimaliza kwa kuwasihi wote watakaonufaika na mradi watumie vyema taarifa zitakazotolewa na kituo
Ungana nami√√√√
No comments:
Post a Comment