Saturday, 8 August 2015

Babake mtoto wa kipalestina aliechomwa afariki


Babake mtoto wa kipalestina aliyechomwa moto hadi akafa juma lililopita na walowezi wa kiyahudi katika maeneo yaliyokaliwa ya ukingo wa magharibi (West Bank) ameaga dunia.
Sa'ad Dawabsheh ameaga dunia katika hospitali ya Soroka iliyoko Israeli.



Babake mtoto Mpalestina aliyechomwa moto akafa ameaga dunia
Bwana Dawabsheh alipelekwa Israeli ilikupata matibabu baada ya kuungua katika shambulizi lililoteketeza mtoto wake mchanga wa mwaka mmoja u nusu.
Shambulizi hilo lililotekelezwa na walowezi wa Kiyahudi lilimuacha bwana Dawabsheh mke wake na mwana wao mwenye umri wa miaka 4 wakiuguza majereha mabaya.
Mke wake bi Riham na mwana wao Ahmad bado wako katika hali mahututi.

Nyumba yao ilichomwa moto katika shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na walowezi wa kiyahudi
Shambulizi hilo lililotokea mwisho wa mwezi Julai liliibua hasira miongoni mwa Wapalestina na wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu ambao waliilaumu Israeli kwa kukosa kuwajibikia usalama wa Wapalestina mikononi mwa Walowezi wa kiyahudi.
Wakati wa shambulizi hilo,Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon alitaka wale waliohusika kwenye shambulizi la kumchoma mtoto Mpalestina katika eneo linalokaliwa na Israel la ukingo wa magharibi kufikishwa mbele ya sheria.

Kifo cha mtoto huyo kiliibua hasira na maandamano
Waziri mkuu wa Israel Benjamin aliahidi kuwa wale waliotekeleza kitendo hicho alichokitaja kuwa cha kigaidi wangechukuliwa hatua za kisheria.
Netanyahu alielezea mshangao wake kutokana ni kile alichokitaja kuwa mauaji ya kikatili alipowatembelea wazazi wa mtoto huyo na nduguye hospitalini.



Source: bbcswahili

No comments:

Post a Comment