Wednesday, 4 February 2015

MASAHA KABLA YA UCHAGUZI MKUU 2015

Ni Mwiaka 53 Tukiwa Tunaongozwa Na Serikali Inayoundwa Na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Katika Awamu Nne, Awamu Ya Kwanza Tuliongozwa Na Hayati Mwl Julias Kambarage Nyerere Awamu Hii Ya Kwanza Ilikuwa Ya Kusifika. Awamu Ya Pili Tukawa Na Mh Mwinyi Mzee Wa Ruksa. Awamu Ya Tatu Mh Benjamin Mkapa Ambae Alisifika Kwa Kuimarisha Uchumi, Japo Wananchi Walianza Kupoteza Imani Na Chama. Na Katika Awamu Hii Tuliyonayo Tupo Na Mh Jakaya Kikwete Ambae Amepata Changamoto Nyingi Zilizowafanya Wengi Kukata Tamaa Na Chama Hiki Kilichoridhi Damu Ya TANU Iliyotutafutia Uhuru Kutoka Kwa jkkWakoloni. Ni Nafasi Yetu Kutafakari Ni Uongozi Upi Unatufaa. ANGALIZO KWA VYAMA. 1.Kutokana Na Wananchi Wa Tanzania Kuelimika Na Kuwa Wachunguzi Wa Hali Ya Juu Yapasa Chama Kijipange Kwa Sera Zinazotekelezeka. 2. Chama Chochote Cha Siasa Kumwandaa Mgombea Anaetarajiwa Na Wengi Na Kuungwa Mkono Ili Kuweza Kupata Ushindi Usio Na Doa. 3. Chama Chochote Kiandae Na Kufanya Kampeni Zake Kistaharabu Pasipo Kuingiliana Kwa Namna Yoyote Ile Itakayosababisha Uvunjifu Wa Amani. 4. Chama Chochote Kihakikishe Wapiga Kura Wanapata Haki Ya Msingi Ya Kujiandikisha Kwa Kutoa Elimu Zaidi.( Kwa Kuzingatia Tutakuwa Na Mfumo Mpya Wa BVR). 5. Chama Chochote Kielewe Kinaongea Na Watanzania Wasomi Ambao Wanahoji Kila Herufi Itokayo Mdomoni Kwa Mgombea Au Kiongozi. Hapa Namaanisha Kuongea Pasipo Kuropoka. 6. Chama Chochote Kiwe Tayari Kujibu Maswali Magumu Yatakayojitokeza Popote Kukiusu,Ikiwemo Kwenye Mitandao Ya Kijamii. Hii Itakisaidia Kuaminiwa. 7. Chama Chochote Kiwe Na Utoaji Wa Elimu Maalumu Ya Kuheshimu Na Kutii Sheria.Pia Walitake Jeshi la Polisi Kufanya Kazi Katika Taratibu Na Sheria. 8. Chama Chochote Kikiona Makosa Popote Kitoe Msahada Ili Kuweza Kupatia Ufumbuzi Ambao Utafanya Kila Kitu Kiwe Sawa Kama Kilivopangwa. 9. Chama Chochote Kijitaidi Kutumia Lugha Inayoeleweka Katika Utoaji Wa Sera Ili Kundi Kubwa Liweze Kuelewa Na Kuzichambua. Kitendo Hiki Kitafanya Kila Mtu Ajue Anapigia Nini Au Nani Na Kwa Sababu Gani. 10. Ni Vema Na Sisi Raia Tukawa Watulivu Katika Kuitafuta Tanzania Iliyo Bora Itakayokua Mfano Wa Kuigwa Katika Nyanja Zote. Uchumi Imara, Siasa Bora, Ulinzi Na Usalama Ulioimarika NK

No comments:

Post a Comment