Wasanii wa kundi la Jambo Squad kutoka Arusha wamethibitisha kauli ya kuwa muziki unalipa baada ya kufungua mgahawa jijini humo.
Jambo Squad wamedai kuwa licha ya kuonekana wanafanya muziki wa tofauti, wameweza kupiga hatua kimaisha.
“Sisi ni watoto wa uswahilini, tumelelewa uswahilini so maisha tunayajua,” waliiambia XXL ya Clouds FM.
“Sisi ni watu wa biashara sio kukaakaa tu. Ila kwa sasa hivi tumeamua tuanzishe sehemu ambayo itatukutanisha na watu wetu ambayo ni CafĂ©. Ni biashara ambayo itaingiza pesa kila siku, ndio tukaamua kufungua Cafe. Ipo maeneo ya Sakina, ambapo ni karibu na Jambo Squad Camp.”
Wamedai kuwa mgahawahi huo umewagharimu fedha nyingi kuuanzisha, hali ambayo inadhiirisha muziki wa kitanzania unalipa tofauti na wengi walivyoamini nyakati za nyuma.
No comments:
Post a Comment