Wednesday, 9 September 2015

Nashangazwa na Magufuli kushangazwa na mambo ya Chama chake.







Mwaka huu ni Mwaka ambao Tanzania inatarajia kuandika historia nyingine mpya ya Taifa hili ikiwa ni mwaka ambao waTanzania wataamua hatma ya nani au chama gani kitaunda serikali ya awamu ya tano tangu kupata uhuru miaka 53 iliyopita.

Chama cha Mapinduzi ambacho ni zao la TANU kimekuwa kikiaminiwa na watanzania kwa miaka mingi sana kwa utendaji wake, japo kwa siku za hivi karibuni vyama vya upinzani vimeonekana kuimarika sana kwa kujengea hoja madhaifu ya Serikali.

Nije kwenye lengo la kuchukua kalamu yangu, Dr John Pombe Magufuli ni mgombea uraisi kwa tiketi ya chama cha mapinduzi na tumemshuhudia akizunguka mikoani kunadi ilani za chama chake ambacho bado kimekamatia dola.

Katika hali isiyo ya kawaida ameonekana kushangazwa na mambo mengi ambayo yanafanywa na serikali inayoundwa na chama kilichomteua, Mavhache kati ya mengi aliyoonyesha kushangazwa nayo ni;

×Kukosekana kwa dawa katika hospitali za serikali wakati za binafsi dawa zipo.

×Mama Ntilie kuteswa na mgambo.

×Waendesha pikipiki za miguu miwili (Bodaboda) kukamatwa ovyo.

×Anashangazwa shule kukosa madawati. N.k

Naweza kumwambia hata mimi nashangazwa na yeye kushangazwa na mambo ambayo yeye anahusika kuunda serikali, yupo katika baraza la mawaziri na pia M/kiti wake wa Taifa ndie Rais wetu ambae wakiwa katika vikao vya kichama anaweza kumshauri.

Katika hali nyingine naweza kumuuliza je kama yeye aliepo ndani ya serikali ameshangazwa na kinachofanywa na serikali je sisi wananchi tujaribu kuwapa nafasi wale ambao hawajawahi kuunda serikali tuone kama wao ndio wataaacha kumshangaza???

Ni kweli changamoto haziwezi kuisha lakini kuzipunguza inafaa kupungua.Kabla wino haujaniishia naomba nimongezee mengine ya kumshangaza;

•Twiga kupanda ndege pamoja na ukubwa wote ule.

•Kushuka kwa shiligi yetu kwa poromoko kubwa sana kwa kipindi cha miaka kadhaa.

•Kupanda kwa uchumi wa taifa huku baadhi watanzania wakishindwa kumudu gharama za milo mitatu kwa siku.

•Naomba ushangazwe na mtanzania anaeweza kusema 20 million ilikuwa pesa ya mboga wakati huo kuna mwingine anaepigwa na mgambo kwa kuuza ndizi apate angalau tsh 100 ya barafu ipooze koo.

Katika yote yanayokushangaza sisi wananchi ndio tulipaswa kushangazwa nayo tukuhoji wewe ila kwa kuwa na wewe unashangazwa nayo naomba tutafute mtu atakaekuwa na majibu ya yanayokushangaza ayatatue.

Mwisho kabisa nikgusihi na nikushauri kwa dhati kabisa  kuwa tumeona vyama vinne vimeunganisha nguvu ili kupata suluhisho la yanayotushangaza na kukushangaza pia, hivyo basi kama unashangazwa kweli kutoka moyoni ungana nao ili mshangazwe wote mkiwa kitu kimoja mtafute suhuu stahiki.

Ni maoni yangu machache kwa mwenendo wa kampeni za Chama changu hadi kufikia zilipo leo. Ukiona wanasema amenunuliwa ujue ni wa muhimu ndio maana kanunuliwa.


No comments:

Post a Comment