Saturday, 12 September 2015

Muigizaji ambae pia ni mbunge nchini Nigeria Desmond Elliot ameongelea hatma ya uigizaji wake


Muigizaji maarufu wa Nollywood ambaye sasa ni Mbunge, Desmond Elliot amesema kuwa kwa sasa anapumzika kufanya filamu ili ajikite vema kwenye siasa.



Amesema kuwa halitakuwa jambo la busara kuchanganya mambo ya uigizaji na maisha yake mapya ya siasa.

“Kazi ya ubunge sio rahisi, nitaonekana sio muwajibikaji kama nitaendelea kuigiza huku nina majukumu mengi ya ubunge” Desmond aliiambia Myjoyonline.

Desmond alijitosa kwenye siasa mwaka 2014 na kugombea Ubunge (Lagos State of Assembly) kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, ambapo alishinda kupitia chama chake cha APC.

Ilani ya uchaguzi ya CCM 2015-2020

Hii hapa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2015-2020. Click hapa kuidownload Ilani CCM 

Friday, 11 September 2015

Full interview ya Tommy Thomas na Evance Lyatuu.

Nimekuwekea interview  kati ya Msanii Tommy Thomas na Exelent Boy Evance Lyatuu iliyofanyika Moshi Fm katika kipindi cha Top fleva kinachofanyika kila ijumaa.
Tommy Thomas akiwa katika pozi kali.

Tommy Thomas akiwa amesimama ndani ya studio namba 2 za Moshi Fm tayari kwa interview katikati ni Shadrack Mafie na wakwanza ni Simon Salvatory wakifatilia mahojiano.

Moja kati ya mambo aliyofunguka ni kuhusu ishu kugombana na maproduser amapo amesema ni kweli amewahi kugombana na moja kati ya produser wake kwa kuwa alikuwa akizungushwa sana kwa kitendo cha kuambiwa kuwa asubiri kila akitaka kufanyiwa kazi. Akaongeza kuwa ilishafikia hatua ya kurekodi pembeni kukiwa na polisi.


Pia Tommy Thomas  anaetamba na nyimbo  yake mpya ya Twende aliyoshirikiana na Wolter Chilambo ameweka wazi wazo lake la kutoa video ya wimbo wake hivyo mashabiki wake wajiandae kupata mambo mazuri kutoka kwake.


× Mazingira aliyokulia nje ya muziki
×Amezungumziwa na ishu ya wimbo wa Roma Mkatoliki kufungiwa.
×Pia amemtaja nani anafaa kuwa raisi yote hayo yapo katika audio hii Click hapa  FULL INTERVIEW  kuisikiliza.

New Song: Tommy Thomas ft Wolter Chilambo-Twende


Nimekuwekea brand new song kutoka kwa msanii wa HIP HOP kutoka Mkoani Kilimanjaro wa kuitwa Tommy Thomas akiwa ameshirikiana na Wolter Chilambo. Wimbo unaoenda kwa jina "Twende" alifanyikia katika studio za Frezzo record mikono ya Aidan machord. click  HAPA KUDOWNLOAD  Tommy Thomas ft Wolter Chilambo-Twende.

Wednesday, 9 September 2015

New Video: Mo Music-Nitazoea



Mo Music ameamua kufuta kiu ya mashabiki wake waliokuwa wakisubiri kwa shahuku kubwa video ya single yake anayotamba nayo inayoenda kwa jina nitazoea.

Jana msanii huyo aliamua kuachia exclusive video hiyo. Kuipata unaweza kubofya HAPA KUDOWNLOAD pia unaweza kushirikisha na wengine.

Nashangazwa na Magufuli kushangazwa na mambo ya Chama chake.







Mwaka huu ni Mwaka ambao Tanzania inatarajia kuandika historia nyingine mpya ya Taifa hili ikiwa ni mwaka ambao waTanzania wataamua hatma ya nani au chama gani kitaunda serikali ya awamu ya tano tangu kupata uhuru miaka 53 iliyopita.

Chama cha Mapinduzi ambacho ni zao la TANU kimekuwa kikiaminiwa na watanzania kwa miaka mingi sana kwa utendaji wake, japo kwa siku za hivi karibuni vyama vya upinzani vimeonekana kuimarika sana kwa kujengea hoja madhaifu ya Serikali.

Nije kwenye lengo la kuchukua kalamu yangu, Dr John Pombe Magufuli ni mgombea uraisi kwa tiketi ya chama cha mapinduzi na tumemshuhudia akizunguka mikoani kunadi ilani za chama chake ambacho bado kimekamatia dola.

Katika hali isiyo ya kawaida ameonekana kushangazwa na mambo mengi ambayo yanafanywa na serikali inayoundwa na chama kilichomteua, Mavhache kati ya mengi aliyoonyesha kushangazwa nayo ni;

×Kukosekana kwa dawa katika hospitali za serikali wakati za binafsi dawa zipo.

×Mama Ntilie kuteswa na mgambo.

×Waendesha pikipiki za miguu miwili (Bodaboda) kukamatwa ovyo.

×Anashangazwa shule kukosa madawati. N.k

Naweza kumwambia hata mimi nashangazwa na yeye kushangazwa na mambo ambayo yeye anahusika kuunda serikali, yupo katika baraza la mawaziri na pia M/kiti wake wa Taifa ndie Rais wetu ambae wakiwa katika vikao vya kichama anaweza kumshauri.

Katika hali nyingine naweza kumuuliza je kama yeye aliepo ndani ya serikali ameshangazwa na kinachofanywa na serikali je sisi wananchi tujaribu kuwapa nafasi wale ambao hawajawahi kuunda serikali tuone kama wao ndio wataaacha kumshangaza???

Ni kweli changamoto haziwezi kuisha lakini kuzipunguza inafaa kupungua.Kabla wino haujaniishia naomba nimongezee mengine ya kumshangaza;

•Twiga kupanda ndege pamoja na ukubwa wote ule.

•Kushuka kwa shiligi yetu kwa poromoko kubwa sana kwa kipindi cha miaka kadhaa.

•Kupanda kwa uchumi wa taifa huku baadhi watanzania wakishindwa kumudu gharama za milo mitatu kwa siku.

•Naomba ushangazwe na mtanzania anaeweza kusema 20 million ilikuwa pesa ya mboga wakati huo kuna mwingine anaepigwa na mgambo kwa kuuza ndizi apate angalau tsh 100 ya barafu ipooze koo.

Katika yote yanayokushangaza sisi wananchi ndio tulipaswa kushangazwa nayo tukuhoji wewe ila kwa kuwa na wewe unashangazwa nayo naomba tutafute mtu atakaekuwa na majibu ya yanayokushangaza ayatatue.

Mwisho kabisa nikgusihi na nikushauri kwa dhati kabisa  kuwa tumeona vyama vinne vimeunganisha nguvu ili kupata suluhisho la yanayotushangaza na kukushangaza pia, hivyo basi kama unashangazwa kweli kutoka moyoni ungana nao ili mshangazwe wote mkiwa kitu kimoja mtafute suhuu stahiki.

Ni maoni yangu machache kwa mwenendo wa kampeni za Chama changu hadi kufikia zilipo leo. Ukiona wanasema amenunuliwa ujue ni wa muhimu ndio maana kanunuliwa.


Diamond atajwa kuwania MTV Europe Music Awards 2015 (MTV EMA)

Diamond Platnumz kwa mara nyingine amepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye tuzo kubwa za kimataifaa.


Ametangazwa kuwania tuzo za MTV Europe Music Awards 2015 (MTV EMA) katika kipengele cha Best African Act.


Wasanii wengine wa Afrika ambao atachuana nao kwenye kipengele hicho ni AKA (South Africa), Yemi Alade (Nigeria), Davido (Nigeria).

Hata hivyo bado anatafutwa msanii mmoja kukamilisha idadi ya nominees watano katika kipengele hicho, ambaye atapatikana kwa kura za mashabiki kupitia Twitter.

Wasanii ambao wametajwa na MTV wapigiwe kura ili apatikane mmoja ni Wizkid (Nigeria), K.O (South Africa), Stonebwoy (Ghana), Cassper Nyovest (South Africa) pamoja na Dj Arafat (Côte d’Ivoire). Kura zinapokelewa hadi September 14 saa 23:59

2015 MTV EMAs zitafanyika Octoba 25, 2015 jijini Milan, Italy ikiwa ni mara ya tatu kufanyika nchini humo na mara ya pili kufanyika kwenye jiji la Milan.

Download Nick Mbishi- Edo. (Audio)

Tumeshuhudia wasanii wengi wa bongo Movie na Bongo fleva wakijitokeza kuonyesha kumsapoti mgombea/Chama fulani cha siasa ikiwemo kwa kuwapigia kampeni majukwaani na kwa kutumia mitandao ya kijamii waliyomo.

Wamo waliojitolea kutumia vipaji vyao vya kisanaa kutoa sapoti kwa baadhi ya wagombea hao. HApa nimekuwekea wimbo wa Nicki Mbishi  aliomwimbia  mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA kwa mwavuli wa UKAWA Hm. Edward Lowassa. Click HAPA KUDOWNLOAD kusikia aliyoyasema Nick Mbishi

Tuesday, 8 September 2015

BASATA yatoa kauli baada ya kuwapo kwa minong'ono kuwa Shilole kafanya show.




Katibu Mtendaji wa baraza la sanaa la taifa (BASATA), Geofrey Mngereza ameiambia Radio 5 ya Arusha kuwa adhabu aliyopewa Shilole ya kufungiwa kutojihusisha kwenye masuala ya sanaa kwa mwaka mmoja haijafutwa.

Mngereza alidai kuwa adhabu iliyotolewa kwa Shilole imetokana na sheria na kanuni zilizotokana na bunge na kwamba kwa sasa wanakusanya ushahidi ili kuchukua hatua.

“Litachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazosema,” alisema Mngereza.

“Kwahiyo itapitia process ile ile ambayo imetumika hapo awali kuweza kutoa adhabu. Kwahiyo ni kitu ambacho kinafanyiwa kazi.”

Nimekuwekea aliyoyasema katibu mtendaji wa Nacte kuhusu mtihani wa darasa la saba.


Katibu mtendaji wa baraza la mitihani (NACTE) Dk. Charles Msonde akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar-es-salaam


Wanafunzi 775,729 walioandikishwa kufanya mtihani wa darasa la saba nchini, kesho wanaanza kufanya mtihani huo, huku idadi ya watahiniwa ikipungua ukilinganisha na walioandikishwa mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es-salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Charles Msonde amesema masomo yatakayotahiniwa kesho na kesho kutwa ni Kiswahili, Kiingereza, Sayansi, Hisabati na Maarifa ya Jamii.

Dk Msonde amesema watahiniwa 748,514 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 27,215 watafanya mtihani huo kwa lugha ya Kiingereza ambayo wamekuwa wakiitumia kujifunzia.

“Watahiniwa wasioona walioandikishwa kufanya mitihani ni 76 na watahiniwa wenye uoni hafifu ambao wanahitaji maandishi makubwa ni 698, kati yao wavulana ni 330 na wasichana ni 368,” alisema Dk Msonde.

Amesema maandalizi ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa fomu maalumu za kujibia mtihani (OMR) na nyaraka nyingine zinazohusu mtihani huo. Alisisitiza kuwa mtihani huo unalenga kupima uelewa wa wanafunzi kwa yale waliyojifunza katika kipindi cha miaka saba.

Katibu huyo wa Necta alizitaka Kamati za Mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa mazingira ya vituo vya mitihani yapo salama, tulivu na kuzuia mianya yote inayoweza kusababisha udanganyifu.

“Mtihani huu ni muhimu kwa Taifa kwa sababu hutumika katika uchaguzi wa wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari. Ni matarajio yetu kwamba wanafunzi wataufanya mtihani huo kwa kuzingatia taratibu zote za mtihani ili matokeo yaonyeshe uwezo wao,” alisema.

Sheria ya ndoa ya kanisa Katoliki huenda ikabadilika na kuwa hivi.


Jopo la wanasheria wa kanisa Katoliki lililoundwa mwaka jana na Papa Fransisi kwa lengo la kupitia sheria za kanisa hilo

Papa Francis anatarajia kurahisisha taratibu zinazoruhusu wafuasi wa kanisa katoliki waliooana kutoa talaka na kuolewa tena huku wakibakia kuwa wafuasi wa katika kanisa hilo .
Maelezo ya taratibu hizo yanatarajiwa kutangazwa mjini Vatcan baadaye leo .
Papa aliunda tume ya wanasheria wa kanisa mwaka jana kupiga msasa mbinu ya kurekebisha taratibu hizo zinazoruhusu wanandoa kuachana na kupunguza gharama .

Papa aliunda tume ya wanasheria wa kanisa mwaka jana kupiga msasa
Bila sheria hiyo wanandoa wa kikatoliki wanaotalikiana na kuolewa upya hutazamwa kama wazinifu na hawaruhusiwi kupokea komunio.

Papa Francis hatabadilisha mafunzo ya katoliki kuhusu kuachana kwa wanandoa , lakini atawezesha kurahisisha wanandoa wenye matatizo kuthibitisha kuwa ndoa yao haikuwa ya maana tangu mwanzo.

Chanzo: bbcswahili

Ulikuwa umeipata hii iliyowakuta wafuasi wa CCM kule Morogoro?? iko hapa




Watu wawili wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na mkanyagano uliotokea juzi Uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli.

Tayari jana, Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete  amewatembelea majeruhi hao waliolazwa Hospitali ya Mkoa Morogoro.

Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Ritha Lyamuya amesema walipokea watu 19 waliokuwa na majeraha yakiwemo ya kuvunjika maeneo mbalimbali ya mwili na kuongeza kuwa miongoni mwao, wawili walikufa kutokana na kuumia vibaya.

Aidha Dk Lyamuya alisema kuwa wagonjwa ambao bado wamelazwa wako 10 na wengine saba walitibiwa na kuruhusiwa.

Dk Lyamuya alisema kuwa waliokufa ni pamoja na mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 42 na mtoto wa umri wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhan Abdalah.

Uwanja wa Jamhuri juzi ulifurika watu wakati mgombea urais kwa tiketi ya CCM John Magufuli alipokwenda kwa ajili ya kufanya kampeni.

Mara tu baada ya Magufuli na viongozi wengine kuondoka uwanjani hapo, ndipo hali ya kusukumana na kukanyagana ilitokea getini wakati watu wakitoka.

Full story kuhusu ziara ya Lowassa jana jijini Dar





Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amesema hakutakuwa na muda wa kupoteza iwapo atachaguliwa akisema ataanza kushughulikia ahadi zote ikiwamo ya ujenzi wa viwanda kwa ajili ya kutatua tatizo la ajira mara tu baada ya kuapishwa.

Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara, Bunju na baadaye Mbezi mkoani Dar es Salaam, Lowassa alisema kila alichoahidi ataanza kukifanyia kazi punde tu baada ya kuapishwa: “Nitajenga viwanda kukabiliana na ajira, ada za shule na mengine ndani ya siku hizo.

“Nikiingia madarakani, hakuna mgeni atakayefanya biashara bila kuingia ubia na wazawa. Lazima tuwajali vijana wetu kwa kuwajengea mazingira wezeshi,” alisema mgombea huyo aliyewasili Bunju saa 9.30 alasiri akitokea Tabora.

Ili kufanikisha hayo, aliwataka vijana kulinda kura zao siku ya uchaguzi ili zisiibwe.

Akizungumza katika mkutano wake uliofanyika kwenye Uwanja cha Shule ya Msingi Bunju ‘A’, Lowassa alisema wananchi wana wasiwasi na NEC kwamba haitatenda haki kwa sababu ya ukaribu wake na CCM.

Aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kufanya kazi mbili, kwanza kupiga kura na pili ni kulinda kura zao huku akisisitiza kwamba ana uhakika kwamba hataibiwa kura ng’o.

Aliwataka wananchi kufanya uamuzi mgumu kuiondoa CCM madarakani ili wajihakikishie huduma bora za jamii katika serikali ya awamu ya tano.

Alisema zimebaki siku 48 kwa wananchi kuamua hatima ya maisha yao yajayo akiwataka kuwachagua wagombea wa Ukawa ili waondoe msongamano wa magari jijini, kuboresha mfumo wa elimu kuanzisha viwanda vitakavyotengeneza ajira kwa wananchi.

Awali, akimkaribisha Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye alisema ili kuepuka vurugu, lazima CCM wakubali kushindwa na kupisha serikali mpya ya Ukawa.

Alisisitiza kuwa ameihama CCM baada ya kubaini kuwa mabadiliko hayawezi kupatikana ndani ya chama hicho.

Alimtaka mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli kuzungumzia kashfa mbalimbali zinazoikabili Serikali ya sasa ambazo ni pamoja na usafirishwaji wa twiga, dawa za kulevya na pembe za ndovu.

“Ndani ya CCM huwezi kufanya chochote, CCM ni shida,” alisema Sumaye na kuongeza kuwa uchumi umeshuka tofauti na miaka 10 iliyopita.

Alisema Ukawa ikiingia madarakani, itahakikisha fedha zote zilizofichwa nje ya nchi zinarudishwa na wahusika wake kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema: “NEC watasababisha machafuko kwa kuibeba CCM. Chama hicho kwa sasa hakibebeki, sasa wameanza kuwatumia watu kumchafua Lowassa.”

Alisema ziara ya kampeni za umoja huo katika mikoa saba, imeonyesha kwamba wananchi wako tayari kwa mabadiliko na kuipokea serikali ya Ukawa.

Awali, mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe (Chadema), Halima Mdee alimtaka Lowassa kusaidia kutatua migogoro ya ardhi katika jimbo hilo hasa eneo la Boko.

Alisema uhakiki wa majina katika daftari la kudumu linaendeshwa kihuni kwa sababu wananchi wakienda kwenye vituo hawalioni.

Mgombea huyo wa urais alihitimisha kampeni zake Bunju saa 10.30 jioni na kuelekea Mbezi kwa ajili ya mkutano mwingine ambao ulimalizika saa 12.15 jioni.

Akiwa Mbozi

Baada ya kuwasili Mbezi saa 11.15, Lowassa aliwaomba wakazi wa Jimbo la Kibamba wamchague pamoja na mbunge na madiwani wa Ukawa ili waweze kumsaidia kuleta mabadiliko yatakayoboresha maisha ya wananchi.

Alisema kumekuwa na tuhuma nyingi dhidi yake, lakini akasema ataendelea kufanya kampeni za kistaarabu ili kuwaeleza wananchi nini anataka kukifanya.

“Wananikashifu kwa maneno mengi, eti wanashangaa mimi kupanda daladala sasa, lakini hawashangai twiga kupanda ndege,” alisema.

Awali, Sumaye alisema hawezi kujibizana na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba kwa sababu na ataonekana amepungukiwa.

Sumaye alisema Chadema ikishinda uchaguzi, kazi ya kwanza itakuwa kutaifisha na kurudisha fedha zilizowekwa na vigogo wa serikali nje ya nchi.

“Kazi ya kwanza itakuwa kurudisha fedha zilizoibwa na vigogo wa Serikali ya CCM, tutazirudisha na kuziweka katika Haz“Kazi ya kwanza itakuwa kurudisha fedha zilizoibwa na vigogo wa Serikali ya CCM, tutazirudisha na kuziweka katika Hazina yetu,” alisema.

Sumaye ambaye mara kwa mara alitumia kaulimbiu ya “CCM” na wananchi kumjibu ni “shidaaa”, alisema tangu Lowassa ajiuzulu kashfa za ufisadi wa fedha za Serikali umeongezeka.

Mbowe ambaye pia Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, aliwataka wananchi hao kuhakikisha wanatunza vitambulisho vya kupigia kura ili waweze kufanya uamuzi sahihi Oktoba 25.

“Mlivyohamasika mnaonyesha kwamba mmekubali mabadiliko, hivyo jambo la msingi ni kutunza vitambulisho vyenu ili siku ya uchaguzi muweze kuwachagua viongozi wa Ukawa,” alisema.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibamba (Chadema), John Mnyika aliomba kura kwa wagombea wote wa Ukawa ili waweze kuleta maendeleo.

“Umati huu unaonyesha kwamba wananchi mna imani na viongozi wanaogombea kupitia Ukawa, tunaomba mtuchague,” alisema.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia chama hicho, Saed Kubenea aliwaomba wananchi wawachague viongozi wa Ukawa ili waende bungeni kuwatetea wananchi

Ilivyokuwa

Wafuasi wa Ukawa walianza kufika katika Uwanja wa Bunju A tangu saa nne asubuhi wakiwa wamejipamba kwa mavazi ya sare za vyama vinavyounda umoja huo.

Baadhi ya wafuasi hao wakiwa na bendera za vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, muda wote walikuwa wakiimba na kucheza nyimbo za Chadema.

Wafuasi hao walikuwa wakipuliza matarumbeta kwenye barabara inayopita jirani na uwanja huo huku baadhi ya magari yaliyokuwa yakipita eneo hilo, yakiunga mkono kwa kupuliza honi.

Madereva wengi kati ya hao, walikuwa wakinyanyua mikono juu na kuonyesha alama ya vidole viwili ambayo inatumiwa na Chadema.

Wafuasi wa chama hicho walipouona msafara wa Lowassa ukiwasili katika viwanja hivyo saa 9.30 alasiri walishangilia kwa sauti ya juu huku wakiimba rais, rais, rais.

Baada ya mkutano kumalizika kwenye viwanja hivyo na msafara wake kuanza safari ya kuelekea Mbezi, saa 10.40 jioni, karibu kila eneo alikopita, wananchi walionekana wakiwa wamejipanga kando ya barabara wakimshangilia, wengi wao wakionyesha alama ya vidole viwili.

Mbali ya kujipanga barabarani, katika baadhi ya maeneo, wananchi walipanda juu ya miti ili wapate kuuangalia vyema msafara huo ulipitia Goba hadi Mbezi.

Huko Mbezi, wananchi walikuwa wamefurika kwenye uwanja wa mkutano tangu saa nane mchana.

Sababu za kuchelewa


Akizungumzia sababu ya kuchelewa kwa mikutano hiyo ambao wa Bunju ulipangwa kuanza saa nne asubuhi na Mbezi saa tisa alasiri, Mbowe alisema hiyo ilisababishwa na kuunganisha safari jana hiyohiyo kutoka Tabora kupitia Dodoma.

“Tunawaomba radhi kwa kuchelewa kuanza kwa sababu ya safari ndefu,” alisema Mbowe.

Pamoja na mkutano huo kumalizika dakika 15 zaidi ya muda uliowekwa na NEC, Polisi waliokuwapo hawakuonekana kuchukua hatua yoyote.

Monday, 7 September 2015

Jambo Squad wapiga hatua nyingine


Wasanii wa kundi la Jambo Squad kutoka Arusha wamethibitisha kauli ya kuwa muziki unalipa baada ya kufungua mgahawa jijini humo.





Jambo Squad wamedai kuwa licha ya kuonekana wanafanya muziki wa tofauti, wameweza kupiga hatua kimaisha.

“Sisi ni watoto wa uswahilini, tumelelewa uswahilini so maisha tunayajua,” waliiambia XXL ya Clouds FM.

“Sisi ni watu wa biashara sio kukaakaa tu. Ila kwa sasa hivi tumeamua tuanzishe sehemu ambayo itatukutanisha na watu wetu ambayo ni Café. Ni biashara ambayo itaingiza pesa kila siku, ndio tukaamua kufungua Cafe. Ipo maeneo ya Sakina, ambapo ni karibu na Jambo Squad Camp.”

Wamedai kuwa mgahawahi huo umewagharimu fedha nyingi kuuanzisha, hali ambayo inadhiirisha muziki wa kitanzania unalipa tofauti na wengi walivyoamini nyakati za nyuma. 

Sunday, 6 September 2015

Friday, 4 September 2015

Mbaroni kwa kuzidisha dakika 6 katika muda kufanya kampeni.




MGOMBEA ubunge wa Chadema, Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, jana amekamatwa na polisi akidaiwa kuzidisha muda katika mkutano wake wa kampeni na kufanya maandamano bila kibali.

Tukio hilo lilitokea baada ya mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro ambapo Lema alihutubia hadi saa 12:06 badala ya saa 12:00, na aliposhuka jukwaani na kuanza kuondoka, wafuasi wake walianza kumfuata na kusukuma gari lake.

Baada ya hatua chache kutoka uwanjani hapo, polisi walianza kuwatawanya wafuasi hao na baadaye kumkamata Lema na kwenda naye Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Arusha.

Awali katika hotuba yake, Lema alimshukia mpinzani wake, Philemon Mollel wa CCM, kwamba anafanya kampeni zake kwa kutumia mbinu chafu za ukabila na udini.

Katika uzinduzi wake wa kampeni Agosti 23, mwaka huu, mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, alizidisha dakika 36, lakini hakuna hatua yoyote aliyochukuliwa.

SOURCE; MTANZANIA

Wednesday, 2 September 2015

Ijue Zanzibar na vivutio vyake




Na, Baraka Ngofira


Mji mkongwe wa Zanzibar ni mji wenye historia kubwa na jina kubwa sana hasa kwa kusifika katika biashara ya utumwa ambapo kulikuwa na soko kuu la Afrika Mashariki la kuuzia watumwa kutoka katika nchi zinazozunguka Afrika ya mashariki.


 Historia haiishii kutaja tu kama mji huu ni maarufu katika uuzaji na usafirishaji wa watumwa bali pia mji huu unasifika kwa kuwa na watu wengi maarufu ambao kusahaulika katika historia ya dunia ni vigumu kama vile sultan Seyyid Said, Tippu Tip, Siti binti Said ambaye alivuma kwa uimbaji wa taarabu za Kiswahili, pia wapo Shekh Abdallah saleh Farsy ambaye ni mwandishi wa vitabu maarufu na mtafsiri wa Quran katika lugha ya Kiswahili.
Mji huu mkongwe wa Zanzibar sio tu unasifika kwa historia ndefu bali pia ni mji ambao umeingizwa kwenye urithi wa dunia ukiwa na fukwe nzuri za kuvutia, maboma ya kuvutia na yaliyojaa maajabu ikiwemo jumba linalofahamika kama Beit-al-ajaib katika lugha ya kiarabu umaajabu wa jumba ili ni kuwa na nguzo 44 zilizojengwa  kwa umahiri na umaridadi na uimara wa hali ya juu.


Jambo la kufurahisha na kuvutia katika jingo hili ndilo jengo la kwanza Afrika Mashariki na kusini mwa jangwa la sahara kuwa na umeme na lifti, na hivyo kulifanya kuwa jumba la kitalii linalovutia watalii na watu wengine wafikao Zanzibar kwenda kutalii na kutazama jengo hili.
Pia limekuwa kivutio kikubwa kwa watalii kuja kujifunza tamaduni na mambo ya kale na hatua mbalimbali za kimaendeleo zilizo kuwa zikifanyika Zanzibar kwa kale na zinazo endelea mpaka sasa, kwa kweli ufikapo Zanzibar usisite kutembelea kwenye jengo hili la kimaajabu.


Kivutio kingine kinachovutia watu kwenda kutalii Zanzibar ni mji mkongwe wa Zanzibar mji wenye historia kubwa na jina kubwa duniani , mji uliokaliwa na watu wengi, mji wenye majumba mengi ya kitalii , makanisa na misikiti ya kihistiroria yote yanapatikana kwenye mji mkongwe wa Zanzibar.
Nyangumi nao wamekuwa kivutio kikubwa hasa kwa watalii watokao bara na nchi nyingine kuja kupiga picha nyangumi wanaoruka na kuonekana kwa uzuri wakitokea majini na kisha kutumbukia majini. Nyangumi hawa wamewavutia maelfu ya watalii kutembelea Zanzibar na kujionea kwa macho yao na wwengine kubaki midomo wazi wakiwashaa nyangumi hawa jinsi warukavyo na kutumbukia majini, kwa kweli Mungu aliumba ndiyo maneno ambayo uwatoka mara nyingi watu hawa.


Ukiachilia mbali nyangumi uwepo wa fukwe nzuri za kuogelea na kupumuzikia za Kendwa,Mungwi,na kiwengwa ni fukwe nzuri za kuvutia zinazokusanya watu wengi hususani nyakati za jioni na nyakati za sikukuu kama vile za Maulid na zile za Xmass na mwaka mpya . sio tu ni fukwe nzuri pia zina upepo mwanana unaowavutia watu wapate fursa hii hadhimu ya kukaa na wale wawapendao na muda mwingi kubadilisha mawazo.
Pia magofu ya kihistoria , chochoro nazo ni vivutio vikubwa hasa kwa wilaya ya mjini Magharibi ambapo watarii hutumia fursa hii adhimu kutembelea na kushuhudia majengo haya na magofu yaliyojengwa kwa umahili na umaridada na mpaka leo yanahifadhiwa vizuri ili kuendelea kuwavutia watu wote wanaotembelea Zanzibar.


Pia uwepo wa Kima wekundu wanaopatikana kwenye misitu ya Jozani na Ngenzi nao wamekuwa kivutio kikubwa sana hasa kwa watalii wanaofika kutembelea katika misitu hii ya ajabu kujionea wanyama hawa ambao ni adhimu kupatikana bara na katika misitu mingine iliyopo bara na katika nchi nyingine duniani. Kweli maajabu ya kima hawa na rangi zao zimekuwa kivutio kikubwa sana. Uwaangaliapo na hata kupiga picha za kwenda kuonesha watu ambao hawajawahi kuwaaona kima hawa na maajabu yao.

Tuesday, 1 September 2015

Uamisho wa De Gea kwenda Real Madrid wakwama dakika za majeruhi



UHAMISHO wa Pauni Milioni 29 wa Kipa David De Gea kutoka Manchester United kwenda Real Madrid umekwama Dakika za mwisho baada ya Mikataba yake kutokamilika kwa wakati.

Tatizo kubwa ni kuwa Dirisha la Uhamisho huko Spain lilifungwa Jana Saa 7 za Usiku kwa Saa za Tanzania wakati lile la Uingereza Leo ndio mwisho wake, hapo Saa 2 Usiku kwa Saa zetu.

Uhamisho huu wa De Gea ulihusu Kipa huyo kwenda Real na Klabu hiyo ya Spain kuilipa Man United Pauni Milioni 29 pamoja na kumtoa Kipa wao kutoka Costa Rica, Keylor Navas, kwa Man United.

Hivi sasa kila Klabu imebaki kimya lakini ripoti kutoka huko Spain zinadai kuwa Man United ndio waliochelewesha kukamilisha Uhamisho huo kwa kutuma Mkataba uliosainiwa Dakika 1 baada ya Dirisha la Uhamisho kufungwa hapo Saa 7 na Dakika 1 Usiku.

Hata hivyo, habari toka ndani ya Man United zinadai kuwa wanayo Risiti inayoonyesha kuwa Makabrasha yote yalitumwa kwa wakati.

Ikiwa ukweli ni kuchelewa kwa Makabrasha kufika huko Spain kwa wakati basi kilichobaki ni Real kukata Rufaa kwa FIFA ambao ndio wanahusika kwa Uhamisho wa Kimataifa.

Bila hivyo David De Gea atabakia Man United kwa Msimu zaidi hadi Mkataba wake umalizike mwishoni mwa Msimu huu wa 2015/16.

Monday, 31 August 2015

Baada ya Nick Minaj kukutana na Miley Cyrus si akamchimba mkwara. soma zaidi

Nick Minaj (Msanii wa hip hop alichukua tuzo ya video bora ya hip hop -Anaconda)


Miley Cyrus (aliyekuwa MC katika tuzo za MTV)


Moja kati ya vitu vilivyoleta mjadala wakati wa ugawajwi wa Tuzo za MTV kwa upande wa wanamuziki wa Marekani ni pale female rapa Nicki Minaj alipomchana MC wa shguhuli hiyo mwanadada Miley Cyrus.

Miley Cyrus. Na Nicki Minaj walikuwa kwenye ugomvi wa maneno kwa muda mrefu hatimaye wawili hao wakakutana ndani ya tuzo hizo na Miley Cyrus ndiye alikuwa MC usiku huo jumapili august 30.

Nicki Minaj alitwa jukwaani kuchukua tuzo yake ya Video bora ya HipHop (Anaconda) na baada ya kuwashukuru wadau wake alimgeukia Miley Cyrus na kumuuliza kwa nini kila siku anamuongelea vibaya?

Miley Cyrus alizuga na kumpngeza Nicki kwa ushndi huo.Haikuweza kujulikana kama hiyo ishu ilipangwa au la pamoja na kuwa uso wa Nicki ulioekana umekasirika.

Nicki alishuka jukwaani na kuelekea sehemu yake ya kukaa huku ukumbi ukifurika kwa kelele za wageni walifika kutokana na maneno ya Nicki kwenda kwa adui wake Miley Cyrus.

Leo tar 31 Agoust nimekuwekea baadhi ya kurasa za juu magazeti. Endelea

















Saturday, 29 August 2015

Kikwete asema kaulii zinazotolewa na upizani kuwa na uchochezi


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amesema baadhi ya kauli zinazotolewa na Umoja wa Vyama vya Upinzani (Ukawa), zinaashiria uvunjifu wa amani pindi matokeo ya kura yatakapoanishwa baada ya zoezi la upigaji kura Oktoba 25 mwaka huu.

Rais Kikwete alisema baadhi ya kauli hizo zimekuwa zikionyesha wazi viashiria vya uvunjifu wa amani na upotoshaji kwa kundi kubwa la vijana ambao wanapiga kura kwa mara ya kwanza.

Akizungumza wakati akizindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao jijini Dar es Salaam Rais Kikwete alisema;

“Wamediriki kusema wazi bila kificho kwamba patakuwa hapatoshi, hizi ni kauli zinazoashiria uvunjifu wa amani. Tunachokisema CCM ushindi kwetu ni lazima na tutashinda kwa kishindo na kwenda nginja nginja mpaka Ikulu.”

Kikwete alisema CCM imejipanga kuhakikisha inapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao na kuongeza kuwa ili kufanikisha hilo wamepanga kikosi kazi ambacho kitatembea nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, mtu kwa mtu ikiwa kwa sasa tayari wameshaanza kufanya kampeni zao kupitia mtandao ya simu za mkononi.

Katika hafla hiyo ya kuzindua kampeni hiyo inayoratibiwa na msanii wa filamu na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, Rais  Kikwete aliwataka wanawake kaungalia mazuri yote yaliyofanywa na Serikali ya CCM katika kumuinua mwanamke.

Source:mwananchi

Waandamanaji wananaopinga serikali wakusanyika Malaysia


Maelfu ya waandamaji wanaopinga serikali wamekusanyika katika nji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur wakitaka waziri mkuu Najib Razak ajiuzulu kwa madai ya ufisadi yanayomkabili.

Mkutano huu wa hadhara umekuwa ukiendelea kwa siku mbili sasa hata baada ya polisi kuupiga marufuku.
Waandamanaji hao pia walikiuka amri rasmi ya kutovaa nguo za manjano zinazotumika na kundi ambalo limeandaa maandamano hayo.

maandamano hayo yalianzishwa baada ya zaidi ya dola milioni mia moja kupatikana katika akaunti ya kibinafsi ya waziri mkuu. Amesisitiza kuwa pesa hizo zilikuwa za msaada na akakanusha kufanya kosa lolote.



Source: bbcswahili

Mahakama moja Misri yawahukumu jela waandishi watatu wa aljazera.


Mahakama ya Misri imewahukumu waandishi watatu wa kituo cha runinga cha Al jazeera kwenda jela miaka mitatu.

Hukumu hiyo ilitolewa baada ya waandishi hao Mohamed Fahmy, Peter Greste na Baher Mohamed kupatikana na hatia ya kutangaza habari za uongo na kulisaidia kundi la Muslim Brotherhood ambalo kwa sasa linatambuliwa kama kundi la kigaidi.

Baher Mohamed pia alihukumiwa kifungo kingine cha miezi sita.

Hata hivyo mmoja wa waandishi hao Peter Greste, yuko nje ya nchi hiyo baada ya kutimuliwa kutoka nchini kwake tangu mwezi Ferbruari.


Licha ya Nick Minaj kuponda tuzo za MTV amepewa nafasi hii. endelea……


Siku ya jumapili agust 30 ni kilele cha tuzo za MTV kwa wanamuziki wa Marekani na tayari wasanii watakao panda siku hiyo wameshajulikana.

Pamoja na Nicki Minaji kuponda uteuzi wa wasanii ndani ya tuzo hizo mwaka huu, lakini uongozi wa MTV umempa shavu Niki Monaji na yeye ndiye msanii atakaeanza kufanya show siku hiyo.

Nicki Minaj anaungana na baadhi ya wasanii wenzake waliotajwa kufanya onyesho siku hiyo ambao ni Justin Bieber, Mackelmore, Ryan Lewis, Pharrell Williams, Tori Kelly ,A$AP Rocky, Twenty One Pilots, Demi Lovato naNick Jonas.


Tuesday, 25 August 2015

Tunatishwa kisa tumeama chama. Ni kutoka Kilimanjaro




Baadhi ya waliokuwa viongozi wa chama cha mapinduzi waliohamia chama cha demokrasia na maendeleo Chadema mkoa wa Kilimanjaro wamesema wameanza kupokea vitisho vya kuhatarisha usalama wa maisha yao ikiwemo kutekwa na kuteswa.

Hayo yamebainishwa na aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro Bw.Fredy Mushi na aliyekuwa katibu wa fedha na uchumi CCM mkoa wa Kilimanjaro Bw.Paul Matemu wakati wakikabidhiwa kadi za baraza la vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo katika manispaa ya Moshi.

Wamesema pamoja na vitisho ambavyo wameanza kupokea hawataogopa na kwamba wamejiandaa ipasavyo kufanya kampeni za kistaarabu ili kuhakikisha wanapata viongozi bora wenye sifa na kufikia lengo la kuleta mabadiliko ya kweli kupitia vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi(UKAWA).

Mapema akikabidhi kadi kwa wananchama hao mwenyekiti wa baraza la vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema)katika manispaa ya Moshi Bw.Dominick Tarimo amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuahidi kufanya kampeni za kistarabu bila vurugu ili kuhakikisha uchaguzi ambao unatarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu unamalizika kwa amani na utulivu.

Naye katibu wa baraza la vijana Chadema Bw.Deogratius Kiwelu amewataka viongozi wanaotoka chama cha mapinduzi na kujiunga  na chama hicho kufuata sheria na kanuni za chama hicho ili kupata ushindi wa kishindo kuanzia ngazi ya uraisi, wabunge na madiwani.

Anguko la soko la hisa bara asia.


Dunia inamkia siku nyingine ya anguko la soko la hisa huko bara la Asia ambapo Japan katika soko kubwa kabisa duniani la hisa limeanguka leo hii huku kukiwa na hofu ya kuporomoka kwa uchumi nchini China.


Soko la hisa la Japan limeanguka kwa asilimia tatu leo jumanne, huko nako nchini Australia soko la hisa likianguka.

Wawekezaji wamekuwa na wasi wasi kutokana na kuanguka kwa soko la hisa huko china ambalo limeanguka kwa asilimia nane nukta tano anguko ambalo ni kubwa kutokea tangu mwaka 2007.




Chanzo:bbcswahili


Saturday, 8 August 2015

Mgombea usaisi kwa tiketi ya ADC amkaribisha Lipumba.


Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Chifu Lutalosa Yemba, amemkaribisha aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kujiunga na chama hicho.
              Profesa Ibrahimu Lipumba.


Chama hicho juzi kilifanya mkutano wa kuwatambulisha wagombea wake wa nafasi ya urais, Yemba anayewania urais wa muungano na mgombea mwenza wake Said Miraj Abdullah, pia alitambulishwa Hamad Rashid Mohamed, anayewania urasi wa Zanzibar.

Yemba kwenye mkutano huo alisema anaufahamu uwezo wa Lipumba katika siasa, ujasiri na uvumilivu wake, hivyo hatakuwa na kinyongo kufanya naye kazi ya kusukuma mbele gurudumu la siasa za upinzani.

Alisema hakujiunga na chama hicho kwa ajili ya kuwa rais, amejiunga kwa ajili ya kutengeneza dola ya uongozi itakayoondoa dhiki na mateso wanayopata Watanzania, hivyo kutokana na uzowefu alionao katika siasa anaamini watafanikisha hilo kwa ufanisi.

“Walinifukuza mwezi wa sita , mwezi wa nane Lipumba amejing’atua kwenye uongozi, watafahamu sasa kuwa kwenye chama kile kuna udhalimu, namkaribisha Lipumba na ninampongeza kwa uvumilivu wake, ingawa ninaumia kuona kiongozi shupavu aliyekuwa na uwezo wa kuhakikisha wananchi wanaamini katika vyama vingine vya upinzani kukatishwa tamaa na watu wachache wenye uroho wa madaraka, ”alisema Yemba.

Alisema kuwa anaingia katika kinyang’anyiro cha kuwania urais akipambana na chama kimoja tu, CCM, hivyo vilivyobaki hakuna wa kumtisha kwa sababu wenyewe kwa wenyewe wameanza kuvurugana.

“Sisi ADC kama bahari, tunachukua maovu yao tunameza, baadaye tunayatema, wakati ukifika wa kufanya hivyo tutafanya kwa sasa , nawaomba Watanzania mpime kwa makini na kuchagua kiongozi anayefaa.

“Mchagueni asiyekuwa mwizi, fisadi, mnyang’anyi asiye na kashfa na hakuna unapoweza kumpata kiongozi wa namna hiyo zaidi ya ADC, pimeni sikilizeni sera zetu, ilani yetu mtuunge mkono. ”alisema Yemba.

Jana, Yemba alichukua fomu za kuwania urais wa chama hicho, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), huku akiwasisitiza Watanzania kukipa nafasi chama hicho ili kuifanyia nchi mabadiliko ya haki na kuondokana na ukandamizaji.

Kabla ya kufikia uamuzi wa kuchukua fomu Nec, Yemba alinukuliwa akisema kama Lipumba angejitokeza jana, angemwachia nafasi ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano. Hata hivyo kuna taarifa Lipumba alisafiri juzi usiku kwenda nje ya nchi.

Said Miraj Abdulla

Kwa upande wa mgombea mwenza wa chama hicho Said Miraj Abdulla, alisema kuwa anamualika Maalim Seif awaeleze Watanzania anataka nini katika siasa, kwa nini anavuruga utaratibu wa kuwapo kwa upinzani wa kweli.

Alieleza kuwa pamoja na kuunga mkono kilichofanywa na Lipumba kutokana na udhalimu unaofanywa na wanasiasa wachache wanaokatisha tamaa wengine, lakini hafurahi kumuona au kusikia anakaa nje ya ulingo wa siasa.

“Nani asiyejua mchango wa Lipumba katika siasa za upinzani wa nchi, arudi kwenye siasa aje kuendeleza safari aliyoianza mwaka 1995, kukaa kwake nje ya siasa kunapunguza nguvu ya Watanzania kufikia kilele cha mafanikio ya kupata rais atakayejali shida zao, kuwasikiliza, kuwanufaisha na rasilimali zinazopatikana nchini mwao, ”alisema Abdulla.

Hamad Rashid Mohamed

Kwa upande wa mgombea urais wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed, aliwataka wananchi kuwa makini wanaposhabikia vyama na kuviepuka visivyoheshimu Katiba.

Alisema alipokuwa kwenye Bunge la Katiba alisema hakuna upawa wala Ukawa, matokeo yake ndiyo hayo watu wanalumbana, Wazanzibar wanahitaji mabadiliko wamekaa kwenye umasikini usiowahusu kwa sababu hakuna ajira.

Alieleza kuwa kwa wakazi wa Zanzibar wanaohitaji ajira, akijenga viwanda vitano tu hakutakuwa na kijana atakayekosa kazi na huo ndiyo mkakati wake katika miaka mitano ya uongozi.

“Watanzania shabikieni vyama huku mkiwapima wagombea wana nia gani na nyinyi, maslahi yao binafsi au kuwasaidia, maana “Tumbili akimaliza miti anakuja mwilini” kuweni makini, ”alisema.

Babake mtoto wa kipalestina aliechomwa afariki


Babake mtoto wa kipalestina aliyechomwa moto hadi akafa juma lililopita na walowezi wa kiyahudi katika maeneo yaliyokaliwa ya ukingo wa magharibi (West Bank) ameaga dunia.
Sa'ad Dawabsheh ameaga dunia katika hospitali ya Soroka iliyoko Israeli.



Babake mtoto Mpalestina aliyechomwa moto akafa ameaga dunia
Bwana Dawabsheh alipelekwa Israeli ilikupata matibabu baada ya kuungua katika shambulizi lililoteketeza mtoto wake mchanga wa mwaka mmoja u nusu.
Shambulizi hilo lililotekelezwa na walowezi wa Kiyahudi lilimuacha bwana Dawabsheh mke wake na mwana wao mwenye umri wa miaka 4 wakiuguza majereha mabaya.
Mke wake bi Riham na mwana wao Ahmad bado wako katika hali mahututi.

Nyumba yao ilichomwa moto katika shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na walowezi wa kiyahudi
Shambulizi hilo lililotokea mwisho wa mwezi Julai liliibua hasira miongoni mwa Wapalestina na wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu ambao waliilaumu Israeli kwa kukosa kuwajibikia usalama wa Wapalestina mikononi mwa Walowezi wa kiyahudi.
Wakati wa shambulizi hilo,Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon alitaka wale waliohusika kwenye shambulizi la kumchoma mtoto Mpalestina katika eneo linalokaliwa na Israel la ukingo wa magharibi kufikishwa mbele ya sheria.

Kifo cha mtoto huyo kiliibua hasira na maandamano
Waziri mkuu wa Israel Benjamin aliahidi kuwa wale waliotekeleza kitendo hicho alichokitaja kuwa cha kigaidi wangechukuliwa hatua za kisheria.
Netanyahu alielezea mshangao wake kutokana ni kile alichokitaja kuwa mauaji ya kikatili alipowatembelea wazazi wa mtoto huyo na nduguye hospitalini.



Source: bbcswahili

Wednesday, 22 July 2015

Ndesamburo asalimu amri

Aliekuwa mbunge wa jimbo la Moshi Mjini ndg. Felemoni Ndesamburo ameamua kuachia jimbo kwa mtu mwingine. Ni baada ya kutojitokeza kwa kuchukuwa fomu. Waliochukuwa ni hawa.


Makada watatu wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Wilayani moshi wamejitokeza kuomba ridhaa ya chama kuteuliwa kukiwakilisha katika ngazi ya ubunge katika jimbo la Moshi mjini.

Katibu wa chadema manispaa ya Moshi ndg. Steven LubelwaAkizungumza amesema waliochukua na kurejesha fomu kwa wakati ni...

 Eliakunda George,
 Basil Lemul Lema,
 Raphael Japhary Michael.
Pia ndg. Lubelwa alitaharifu chombo hiki kuwa tarehe ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu za ubunge ndani ya chama hicho ilikuwa ni tar 19july hivyo kwa sasa ni kura za maoni zinatarajiwa kufanyika.

Mwana habari alipotaka kujua utaratibu wa kumpata mwakilishi mmoja utakuwaje Katibu Steven Lubelwa alisema Mchakato utahusisha wajumbe kutoka katika kata zote katika jimbo la Moshi Mjini huku akisema mchakato huo utafanyika katika ukumbi wa Uhuru hostel tar 23 siku ya halhamisi.



Kwa matangazo yoyote mnakaribishwa kutangaza nasi kwa bei nafuu. Kwa mawasiliano wasiliana nasi kwa simu +255766442555, au email shadrackmafie@yahoo.com

Sunday, 19 July 2015

Sekeseke la uchaguzi ngazi ya ubunge jimbo la Moshi mjini.

Kuelekea uchaguzi mkuu, wimbi la watangaza nia wanaosaka kupokea bakora la aliekuwa Mbunge wa Moshi mjini Mh. Felemon Ndesamburo linaendelea kuchukuwa sura mpya. Hawa ni baadhi ya wanaolitamani kwa upande wa Chama cha mapinduzi.
 Kada wa chama cha mapinduzi Manispaa ya Moshi Daudi Mrindoko akiwa ameambatana na mkewe katika ofisi za CCM wilaya ya Moshi kuchukuwa Fomu ya kuwania ubunge kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi.



Kada mwingine na mtangaza nia ndg. Priscus Tarimo akikabidhiwa fomu ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya Chama cha mapinduzi katika nafasi ya ubunge katika jimbo la Moshi mjini. 


Priscus akitoa maelezo binafsi kwa katibu msaidizi wa CCM wa wilaya ya Moshi. Mh Donatha Mushi.

Mtia nia mwingine ambae ni mwakilishi wa jamii ya Bantu Unioni Bwana Omary Mwaliko akirejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama cha mapinduzi kumpitisha kukipeperushia bendera katika ngazi ya ubunge jimbo la Moshi mjini, uchaguzi ujao.


EDmund Rutaraka ambae ni naibu kamanda wa vijana CCM Akipokea fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake.

Ikumbukwe kwa mujibu wa ratiba ya Chama cha mapinduzi mwisho wa kuchukuwa na kurudisha fomu ni Jumapili ya tarehe 19 July2015.


Picha na Dixon Busagaga.

Ungana nami kwa matukio yote yanayojiri.

Piga *149*01#kufurahia huduma bomba za vodacom.